Na
Miza Kona na Maryam Kidiko-Maelezo Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Kikosi cha Valantia Zanzibar (KVZ) hakijavamia
eneo la Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mahonda.
Hayo
yamesemwa leo huko Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi
Unguja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum mhe.
Haji Omar Kheri wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Mhe. Jaku
Hashim Ayoub aliyetaka kujua kwa sabaabu gani Kikosi cha Valantia Zanzibar
kimevamia eneo la uwekezaji.
Amesema
maeneo hayo tayari yameshapimwa na serikali kwa ajili ya matumizi ya Kikosi hicho
na eneo hilo sio la kiwanda cha sukari
pia kiwanda hakina haki ya kisheria ya kulitumia.
“Eneo hilo limepimwa na kwa sasa si sehemu ya
shamba la miwa la kiwanda cha Sukari Mahonda na Uongozi wa kiwanda cha Mahonda
unaelewa kuwa sio sehemu yao”, amefahamisha Waziri huyo.
Amesema
kuwa eneo hilo limekuwa la kiulinzi ambalo lilikabidhiwa kikosi cha Valantia (KVZ)
kwa ajili ya kuanzisha Kambi ya Pangatupu ili kuimarisha shughuli za ulinzi
katika maeneo hayo.
Ameeleza
kuwa Serikali imeandaa mpango maalum wa kuwapatia eneo jengine kwa ajili ya kuweza
kujiendeleza na shughuli zao za kiwanda hicho ili kuepukana na upungufu na
usumbufu wa maeneo ya mashamba ya miwa na kudhorotesha uzalishaji kwa
wawekezaji hao.
Wakati
huo huo Naibu Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano Mhe. Issa Haji Gavu amesema
Serikali kupitia Program ya ZUSP inayotekelezwa kupitia Wizara ya Fedha
inakusudia kujenga mitaro ya maji katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar ikiwemo
eneo la Kijangwani ili kuondoa kutuama kwa maji wakati wa mvua katika eneo
hilo.
Akijibu
suala laMwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe. Ali Salum Haji aliyetaka kujua Wizara
imejipanga vipi kumaliza tatizo hilo, Naibu huyo amesema kuwa eneo hilo la
barabara iliyopo mbele ya jengo la Posta, Kijangwani wakati wa mvua hujaa maji
ambayo huwa ni kero kwa wananchi ambao hutumia maeneo hayo kwa shughuli zao.
Ameeleza kuwa tatizo
la kutuama maji linatokana na eneo hilo kukosa mitaro yenye uwezo wa kuchuku
maji yanayokusanyika hapo kutoka maeneo yajuu kwa vile eneo hilo asili yake lipo
bondeni
No comments:
Post a Comment