Balozi Amina Salum Ali
Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.
Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.
Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika Mungu amlaze pema peponi, Amin.
Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania.
Subhanallah! Kumbe huyu Mheshimiwa Amina siku hizi tokea aende USA hajifuniki tena kichwa(havai mtandio anymore?). Kitu gani kimempata Yaa Rabbi. Inshallah Mungu amuongoe asiendelee kutuadhirisha Wazanzibari na utamaduni wetu na Waislamu kwa jumla.
ReplyDeleteMie huko kote siko namjuwa huyu dada kama NI MJUWAVYO dada yangu baada ya kuiona hii picha yake nimejikuta mwenye kufikiri jinsi binadamu tukuwavyo huyu dada leo ameshakuwa mtu mzima Umri umechukuwa nafasi yake Mmungu ampe upeo wakuona mbali kwani Mmungu anatwambia Dunia ni wakati tu na nafsi ni tamaa kama
ReplyDelete