Habari za Punde

Mzee Majuto Awakonga Nyoyo Wananchi wa Zenj Kariakoo.

 
Watoto wakitowa burudani ya kushindania kucheza muziki wakati wa Maonesho ya King Majuto katika viwanja vya Kufurahisha Watoto Kariakoo Zenj, ikiwa ni kuadhimisha Kumbukumbu ya Mzee Abeid Amani Karume. onesho hilo limeandaliwa na Tigo 
Msanii Maarufu wa Vichekezo Zanzibar Halikuniki akitowa burudani ya kichekesho cha Wake wenza wakati wa onesho la kumbukumbu ya Mzee Abeid Amani Karume lililofanyika katika uwanja wa Kufurahisha Watoto Kariakoo Zanzibar.
 Wake wenza wakimngangania mumu wao Mzee Halikuniki wakato wa onesho lao lililofanyika viwanja vya Kufurahisha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Wasanii wa Kikundi cha Dansa cha Kontija wakitowa burudani ya mziki wa dansa wakjati wa onesho hilo katika viwanja vya Watoto Kariakoo Zenj.

King Majuto akitowa burudani ya mchezo wa kutojuwa kusoma jinsi ya hasara yake unayopata kwa jamii inabidi kusomewa barua na kusomewa uongo. 

King Majuto akielimushwa faida ya kusoma wakati wa onesho lake lililofanyika katika viwanja vya Kariakoo Zanzibar lililowashirikisha wasanii wa Zanzibar akiwemo Halikuniki 
                        Dansa wa Kundi la B.Six wakitowa burudani wakati wa onesho hilo.
Watoto wakilishambulia jukwaa kwa kuonesha jinsi ya kucheza muziki wa kizazi kipya wakati wa onesho lililoandaliwa na Kampuni ya Simu ya Tigo katika viwanja vya Kariakoo Zenj.

Hili ilivyokuwa wakati wa onesho la kuadhimisha Siku ya Karume Day katika viwanja vya Watoto Kariakoo Zenj.
              Wasanii wa Kudansa wa Kundi la Kontija Dansa wakifanya vitu vyao jukwaani.



Wananchi waliofika katika viwanja vya Kariakoo wakifuatilia shoo hiyo ya mzee majuto na halikuniki, kabla ya kuaza kwa shoo hiyo kulikuwa na michezo ya kushindanisha watoto kucheza muziki.
Wananchi wa Mji wa Zenj wakiwa kastika viwanja vya watoto wakimshangilia Mzee Majuto wakati wa onesho lake la vichekesho na Msanii wa Zanzibar Halikuniki wakiwa wamefurika katika kiwanja cha kufurahisha Watoto Kariakoo hivi karibu,  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.