Habari za Punde

Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Yatembelea Miradi ya Maendeleo Inayotekelezwa na Idara ya Njia Zanzibar.

 Wajumbe wa kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi wakitembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa  na Idara ya Ujenzi wa Barabara (UUB).  Mwenyekiti wa Kamati hiyo wakwanza (kushoto) Mahmoud Muhammed Mussa akiwa na wajumbe wenzake na watendaji wakuu wa UUB wakikagua barabara ya Chaani iliopo Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja. 
Mhandisi Mkuu  wa UUB  Eng. Cosmas Masolwa akitoa maelezo  kwa wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi  ya Baraza la Wawakilishi juu ya ukarabati unaoendelea wa  kuihami njia ya Chaani kwa kuwekewa kifusi kabla ya kukamilishwa  ujenzi wake kwa kiwango cha lami hap baadae.
Sehemu ya barabara ya Chaani iliyotembelewa na Kamati  hiyo  ambayo inafanyiwa matengenezo ya kutiwa kifusi  ili weze kupitika huku ikisubiri ujenzi wake kwa kiwango cha lami hapo baadae.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.