Habari za Punde

Maalim Seif Afungua Masjid Aqsaa Kiboje Mkwajuni Unguja.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akifungua pazia kuashiria ufunguza rasmi wa MASJID AQSAA katika kijiji cha Kiboja Mkwajuni, Wilaya ya Kati Unguja.
Sheikh Abdalla Rajab, akisoma risala ya wazee wa MASJID AQSAA ulioko Kiboje Mkwajuni wakati wa hafla hiyo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na, viongozi wa dini ya kiislamu nchini pamoja na waislamu mbali mbali wakisikiliza hotuba ya Ijumaa iliyotolewa na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraha (hayupo pichani) katika msikiti mpya wa  MASJID AQSAA ulioko Kiboja Mkwajuni. Kushoto ni Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji akifuatiwa na Mufti Mkuu Sheikh Saleh Omar Kabi.
 Sheikh Thabit Jongo kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, akitoa nasaha baada ya ugunguzi MASJID AQSAA Kiboje Mkwajuni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria  ufunguza wa MASJID AQSAA katika kijiji cha Kiboja Mkwajuni, Wilaya ya Kati Unguja.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, akitoa nasaha baada ya ugunguzi MASJID AQSAA Kiboje Mkwajuni.
 Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu walioshiriki katika ufunguzi wa MASJID AQSAA, Kiboje Mkwajuni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya ugunguzi wa MASJID AQSAA na sala ya Ijumaa katika kijiji cha Kiboje Mkwajuni.(Picha na Salmin Said OMKR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.