JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WATANZANIA
WALIOKUWA AFRIKA KUSINI WAMEREJEA NYUMBANI
Kundi la Watanzania 26
limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini
leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya
wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea
nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.
Watanzania hao walikuwa
wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban.
Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa
wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la
kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania
nchini Afrika Kusini.
Wakati huo huo, Ubalozi wa
Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wengine
wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi
umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa
madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.
MWISHO.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa
Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa,
25 Aprili 2015
No comments:
Post a Comment