Habari za Punde

Kada wa Chama cha Mapinduzi Ansi Mmasi Atoa Msaada kwa Wananchi Walioathirika na Mafuriko Moshi Vijijini.

Chakula cha msaada kwa ajili ya wananchi walio athirika na mafuriko wilaya ya Moshi vijijini kikushushwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ajili ya kwenda kukabidhiwa kwa wahusika.
Kada wa Chama cha Mapinduzi Ansi Mmasi akikabidhi msaada wa Chakula kwa afisa tarafa,Eveline Mmary ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya katibu tawala wa wilaya ya Moshi .
Afisa Tarafa wa Kilimanjaro akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa chakula kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika eneo la TPC wilaya ya Moshi vijijini.
Kada wa chama cha Mapinduzi Ansi Mmasi akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa Chakula kwa ajili ya watu walioathirika na mafuriko katika eneo la TPC wilaya ya Moshi vijijini.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.