Habari za Punde

Waziri na Mwakilshi watimiza ahadi zao kwa TUEPO

 Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Ali (Jazira) akimkabidhi Kompyuta mbili na mashine ya Fotokopi moja Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wasio na ajiri (TUEPO) Ussi Said Suleiman ikiwa ni muendelezo wa ahadi yake aliyoitoa wakati alipoitembelea Jumuiya hiyo iliopo ndani ya Jimbo lake, hafla hiyo imefanyika Skuli ya Rahaleo Mjini Unguja.
 Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii Vijana, Wanawake na Watoto Bi. Zainab Omar Muhammed akimkabidhi shilingi Milioni 1,000,000/- Mwenyekiti (TUEPO) Ussi Said Suleiman kwa ajili ya usajili wa Chuo chake ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati alipoizindua Jumuiya hiyo.
 Baadhi ya wageni walikwa wakifuatilia makabidhiano hayo yaofanyika Skuli ya Rahaleo Mjini Unguja.

Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii Vijana, Wanawake na Watoto Bi. Zainab Omar Muhammed (wakatikati) katika picha ya pamoja na Vijana wa Jumuiya ya Watanzania wasio na ajiri (TUEPO).Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.