STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Pemba
3.7.2015
WANANCHI wa Mkanyageni, Mkoa wa Kusini Pemba
wamepongeza juhudi kubwa zilizochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein za kuhakikisha amani, utulivu
na mshikamano miongoni mwa wananchi vinaimarika kwa lengo la kuleta maendeleo.
Hafla hiyo ya
futari ilifanyika katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni, na kuhudhuriwa na
wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani pamoja na viongozi mbali mbali wa
Mkoa huo pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Aidha, Mama
Mwanamwema Shein naye aliungana pamoja na akina mama wenzake wa kijiji hicho
cha Mkanyageni katika futari hiyo ya pamoja.
Wananchi hao
waliyasema hayo wakati wakitoa neno la shukurani katika futari maalum
walioandaliwa na Alhaj Dk. Shein hapo kijijini kwao Mkanyageni ikiwa ni utamaduni aliouweka wa kufutari nao pamoja kila
ufikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akitoa neno hilo
la shukurani kwa niaba ya wananchi wa Mkanyageni, Maalim Abdalla Yussuf alisema
kuwa katika uongozi wa Alhaj Dk. Shein wananchi wameshuhudia mshikamano mkubwa
sambamba na kuwepo kwa amani na utulivu ambavyo ndio dira ya maendeleo.
Maalim Abdalla
alisema kuwa mbali ya shukurani kwa futari hiyo aliyowaandalia pia, wananchi wa
Mkanyageni wanatoa shukurani za pekee kwa Alhaj Dk. Shein kwa kuifanyia mema
Zanzibar.
Mara baada ya
futari hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Hemed Suleiman Abdalla
alitoa shukurani kwa wananchi wote waliohudhuria katika hafla hiyo.
Alhaj Dk. Shein alieleza
haja ya kuendeleza ushirikiano na mshikamano uliopo miongoni mwa wananchi wa
Zanzibar sambamba na kuendelea kuishi kwa amani na utulivu.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba Bw.Hemed Suleiman wakati alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni katika futari iliyoitayarisha kwa Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba Bi Hanuna Ibrahim Masoud wakati alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni katika futari iliyoitayarisha kwa Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akishiriki katika swala ya magharibi iliyoswalishwa na Sheikh Chumu Salim kabla ya futari iliyoitayarisha kwa Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba jana katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni
Akinamama wa Vijiji tofauti vya Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni
Wananchi na Waislamu wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katikaviwanja vya Skuli ya Mkanyageni
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Viongozi wengine wakiitikia dua iliyoombwa baada ya kufutari pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba jana katika viwanja vya Skuli ya Mkanyagen
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein kushoto) akiagana na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya futari ya pamoja aliyoitayarisha kwa Wananchi wa kijiji hicho jana
No comments:
Post a Comment