Habari za Punde

Balozi Seif akutana na Balozi mdogo wa Oman

Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kufanya mazungumzo yao ya Ushirikiano wa  kuimarisha uhusiano wa Kihistoria wa muda mrefu wa kidugu uliopo baina ya Oman na Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdullah Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis Ame, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdulla Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo yao Balozi Seif kupitia Balozi Mdogo huyo wa Oman aliishukuru Serikali ya Nchi hiyo kwa jitihada inazochukuwa katika kusaidia harakati za Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.

Balozi Seif alisema kwamba Oman yenye uhusiano wa kidugu na kidamu na Zanzibar imekuwa mshirika mkubwa kwa Zanzibar hasa katika masuala ya kusaidia fursa za Elimu ya Juu kwa wanafunzi wa Visiwa vya Zanzibar.

Mapema Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdulla alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Nchi yake itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za kuelekea kwenye maendeleo.

Balozi Ali Abdulla alisema uhusiano wa Kihistoria wa muda mrefu wa Wananchi wa Oman na Zanzibar unatokana na maingiliano ya kidamu yaliyopo  kwa karne nyingi zilizopita kati  ya watu wa pande hizo mbili.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.