Habari za Punde

Shamra Shamra za Kusherehekea Ushindi wa Majimbo ya Wilaya ya Amani Unguja

Washindi wa Jimbo la Mpendae Mbunge na Mwakilishi wakiwasili katika viwanja vya Afisi ya CCM Wilaya ya Mjini Amani kuhudhuria utoaji wa matokeo ya Kura za maoni ya Majimbo yao
Wanachama wa CCM wakisherehekea ushindi wa Wagombea wao wakati wakiwasili katika Afisi ya CCM Wilaya ya Amani kuhudhuria sherehe za utoaji wa majina ya Washindi wa Kura za Maoni katika majimbo yao Matano, Amani, Magomeni, Kwamtipura, Chumbuni na Mpendae. 
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya Afisi ya CCM Wilaya ya Amani kuhudhuria hafla ya utoaji wa Matokeo ya Kura za Maoni.
Mgombea nafasi ya Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar ambye ameshinda kura za maoni katika uchaguzi uliofanyika katika matawi mbalimbali katika jimbo hilo.akishindikizwa na Wananchi wa Jimbo hilo,
 wa 
Mteule wa kugombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar na Kamanda wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza HAMJAD akiwasili katika Afisi za CCMWilaya ya Amani kuhudhuria hafla ya utoaji wa matokeo ya Kura za maoni kwa Majimbo ya Wilaya hiyo.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakisherehekea ushindi wa wagombea wao katika viwanja vya Afisi ya CCM Wilaya ya Amani. 
Mbunge wa Jimbo la Mpendae Mhe Salim Hassan Turky na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza HAMJAD wakipogezana wakati wakiwasili katika Afisi ya CCM Wilaya ya Amani.
Mbunge wa Jimbo la Mpendae Mhe Salim Hassan Turky akimpongeza mgombea nafasi ya ubunge jimbo la Chumbuni kwa ushindi wa kishindo kumshinda mpizani wake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Perera Ame Silima. 
Mgombea Ubunge Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza HAMJAD akipongezwa na mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kwamtipura Ali Juma RAZA wakiwa katika Afisi za CCM Wilaya ya Amani. 
Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya Afisi ya CCM Wilaya ya Amani wakisherehekea ushindi wa Wagombea wao
Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Mpendae na Amani Salim Hassan Turky kushoto Mhe Mussa Hassan Mussa wakibadilishana mawazo wakiwa katika Afisi ya CCM Wilaya ya Amani wakisubiri kutajwa rasmin ushindi wa Wagombea hao.
Mwakilishi wa Mpendae na Mgombea Ubunge wa Chumbuni wakipongezana baada ya ushindi walioupata wakati wa kura ya maoni wakiwa katika Afisi ya CCM Wilaya ya Amani.
Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akiwa na familia yake katika Afisi ya CCM Wilaya ya Amani wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa kura ya maoni katika CCM
Mgombea Ubunge Jimbo la Chumbuni akiwa na familia yake katika jengo la Afisi ya CCM Wilaya ya Amani Unguja. wakiwa na furaha ya ushindi wa ndugu yao
Wagombea wa Ubunge kushoto Mgambea wa Jimbo la Chumbuni Ndg Ussi Salum Pondeza na kulia Mgombea Ubunge Jimbo la Magomeni Ndg Jamal Kassim Ali wakiwa katika Afisi za CCM Wilaya ya Amani Unguja. wakisubiri kutajwa kwa matokeo ya uchaguzi wa kura ya maoni 


2 comments:

  1. Nawaponeza wale wote waliopata nafasi ya kuwakilisha majimbo yao ktk nafasi mbali mbali na M/Mungu awajaalie washinde ktk uchageguzi mkuu juao.

    Tathmini yangu:

    Kati ya majimbo yote ya Wilaya ya Amani, Jimbo la Mpendae ndio la kwanza kwa "kuramba dume" lazma tukubali Turky ni zaidi ya mbungu, huyu ni mwanamaenekeo wa kweli.

    Wakati wateule wa wamajimbo mengine wanatafuta mbinu za kushinda majimbo yao Turkey hana muda huo.

    Wapinzani wakuu wa turkey ktk jimbo (Cuf) wamegawanyika kuhusu suala la mhe Turkey kua mbunge kutoka na juhudi zake za maendeleo jimboni tene bila ya ubaguzi.

    Turkey, kaleta maji, barabara za jimbo, madrassa mbili za kisasa pamoja na misaada ya futari na sikukuu kila ramadhani, tena kila mtu anapewa akapike kwake na sio vurugu la kukusanya watu na kutangazwa na matv...kwa kweli ALLAH AMLIPE!!!

    Ama kwa upande wa ndugu yetu Dimwa yeye ukiwa na shida inayohusu huduma ya kiserikali na kama ni 'mdau' atakusaidia, yeye tunampa tu kwa vile ni "HOME BOY"

    Wengine walioramba 'dume' ni wale wa chumbuni kwa "AMJADI" Mshkaji huyu sio msomi wala mwanasiasa mzuri lkn, naamini atachopata atakuala "na wa kwao" amekua msaada mkubwa kwa jimbo lake hata kabla hajawa mbunge... nadhahani nae tumuombee dua!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.