Na Miza Othman, Maelezo
Uhamiaji haramu umeshamiri katika kijiji cha Chwaka,
wilaya ya kati Unguja, na kupelekea ongezeka la vitendo vya uhalifu
katika shehia hiyo .
Sheha wa shehia ya Chwaka Simai Msaraka Pinja ameleeza
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea kijiji hicho.
Amesema katika
siku za karibuni kumejitokeza wimbi kubwa la kuingia wageni
hasa wakati wa usiku na kuondoka majira ya alfajiri bila kujua malengo
yao na wamejenga dhana kuwa watu hao wanaingiza madawa ya kulevya.
Sheha Simai amesema uongozi wa Shehia
kwa kushirikiana na jeshi la polisi na askari jamii
wameaanzisha uchunguzi wa kujua maeneo wanayofikia watu hao na wenyeji wao ili
kuweza kuwadhibiti..
Amesema baadhi ya vijana wa Shehia
ya chwaka wamekuwa wakishirikiana na wageni hao na tayari
kumejitokeza dalili za vitendo viovu na baadhi wameanza kuathirika na dawa za
kulevya..
Aidha alisema ongezeko la watu katika shehiya
yake ni jambo linampelekea kutojuwa takwimu za uhakika na kupelekea
kukosa mahitaji ya lazima ya wananchi katika shehiya yake.
Aliwataka wananchi kuwa makini katika kijiji
chao na wakiona watu wasio wafahamu wapeleke taarifa
kwa sheha ili kudhibiti wimbi kubwa la ongezeko la wahamiaji haramu
.
Alitowa wito kwa vijana waachane na vikundi
viovu na wajishuhulishe kufanya kazi wakizingatia kuwa vijana
ndio nguvu ya taifa katika nchi.
Aliomba Serikali iweke vidhibiti katika
bandari ndogo ndogo ili wanaoingia na kutoka waweze
kujulikana na watakaovunja sheria za nchi waweze kushukghulikiwa na
vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment