Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi mpya wa Denmark katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Einar Hebogard alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kujitambulisha ,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Balozi mpya wa Denmark katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Einar Hebogard alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kusalimiana na Rais,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi Victoria Mwakasega alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kusalimiana na Rais,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na mgeni wake Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi Victoria Mwakasega alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo na Rais,[Picha na Ikulu.]
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
8.10.2015
RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amezipongeza hatua
za Serikali ya Marekani ya kuahidi na kuhakikisha kuendelea kuiunga mkono
Tanzania ikiwemo Zanzibar katika uendelezaji wa awamu ya pili ya miradi
inayofadhiliwa na Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC).
Dk. Shein aliyasema
hayo leo, huko Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Balozi wa
Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mark Childress.
Katika mazungumzo
hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo wa Marekani kuwa hatua hizo zinaonesha
dhahiri uhusiano mwema na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Marekani hali
ambayo itaimarisha na kukuza zaidi uimarishaji wa sekta za maendeleo kwa upande
wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Dk. Shein alisema kuwa
azma ya Marekani ya kuendelea kuiunga mkono Tazania katika kuendeleza awamu ya
pili ya Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) ni heshima kubwa kwa Tanzania kwani
ni miongoni mwa nchi chache zilizopata bahati za kuendelea katika awamu hiyo ya
pili ya MCC.
Pamoja na hayo, Dk.
Shein aliipongeza nchi hiyo kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha
miradi mbali mbali ya maendeleo hapa nchini.
Nae Balozi Mark
Childress alimuhakikishia Dk. Shein kuwa awamu ya pili ya Mfuko wa MCC
itatekelezwa na nchi yake na tayari fedha zake zimeshatengwa kwa ajili ya
miradi mbali mbali itakayotekelezwa na Mfuko huo kwa Zanzibar na Tanzania Bara.
Balozi Childress
alitumia fursa hiyo kumueleza Dk. Shein kuwa nchi yake inathamini uhusiano na
ushirikiano mkubwa uliopo kati yake na Tanzania ikiwemo Zanzibar na kuahidi
kuuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo.
Pamoja na hayo Balozi
huyo wa Marekani alimueleza Dk. Shein kuwa hatua nzuri imefikiwa na Marekani
katika kutekeleza azma yake ya ujenzi wa
maabara ya kisasa huko kisiwani Pemba unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Dk. Shein pia alitukutana
na Balozi wa Sweden katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt
na kumueleza kuwa Zanzibar inathamini uhusiano na ushirikiano na nchi hiyo hasa
katika kuimarisha sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya afya ambapo Sweden
imekuwa ikiiunga mkono Zanzibar kwa muda mrefu
Wakati huo huo Dk.
Shein alifanya mazungumzo na Balozi mpya wa Denmark katika Jamhuri ya Muungano
wa Tanzani na kumueleza jinsi Zanzibar inavyothamini uhusiano na ushirikiano
mzuri uliopo kati ya pande mbili hizo.
Dk. Shein aliipongeza
Denmark kwa kuisaidia Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeo ikiwemo sekta
ya elimu kwa kupitia Shirika lake la Maendeleo la DANIDA.
Kwa nyakati tofauti wa
mazungumzo ya Mabalozi hao na Rais Dk. Shein, Mabalozi hao walitumia fursa hiyo
kumpongeza Dk. Shein kwa kuiongoza vyema na mashirikianom mazuri Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa.
Pia, Dk. Shein
alifanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Malawi Mhe. Victoria Mwakasege aliefika Ikulu kwa ajili ya kuaga ambapo katika
mazunguzo yao, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania na Malawi zina
uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu hivyo kuna kila sababu za kuuimarisha.
Dk. Shein alimueleza Balozi huyo haja ya kuimarisha
uchumi wa Kidiplomasia kwa kuishajiisha sekta ya utalii, uwekezaji na biashara
kati pamoja na kuitangaza lugha ya Kiswahili nchini Malawi kwa kuzingatia kuwa
kiswahili kimekuwa kikisomesha hadi vyuo vikuu hapa nchini vikiwemo Chuo Kikuu
cha Dar-es-Salama na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwaeleza Mabalozi
hao kuwa uchaguzi mkuu ujao utakuwa huru, wa haki na utakuwa wa amani na
utulivu mkubwa .
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment