Habari za Punde

TANZANIA YASHUKURIWA KWA KUSAIDIA KUREJESHA AMANI KWA BAADHI YA MAENEO YA MASHARIKI MWA DRC

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa MONUSCO, Bw. Martin Kobler akisisitiza jambo wakati wa mazugumzo yake na  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania,  Balozi Tuvako Manongi. Bw. Kobler alifika katika Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu, kuishukuru Tanzania kwa mchango wake wa ulinzi wa amani katika Mashariki ya DRC. Mchango ambao amesema umeleta tofauti kubwa.
."Tafadhali nifikishie salamu  na shukrani zangu  kwa Mhe. Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Waziri wa Ulinzi" maneno ya  Bw. Martin Kobler kwa Balozi Manongi walipokuwa wakiagana  baada ya mazungumzo yao mwishoni mwa wiki. 

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.