Habari za Punde

Hitma ya Kuwaombea Dua Waumini waliotangulia mbele ya haki Msikiti wa Ijumaa Kidombo

 Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi wa Pili kutoka Kushoto akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa kwanza kutoka kushoto wakijumuika na waislamu katika Hitma ya Kuwaombea Dua Waumini waliotangulia mbele ya haki hapo Msikiti wa Ijumaa Kidombo Kijijini kwa Rais Mstahafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Dr. Samlin Amour.

Wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kanal Mstaafu Juma Kassim Tindwa, Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania Dr. Moha’d Gharib Bilal na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi


 Waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka sehemu mbali mbali Nchini wakihitimisha Hitma ya kuwaombea waislamu walitangulia mbele ya haki hapo kwenye Msikiti wa Ijumaa Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja Kijiji alipozaliwa Rais Mstahafu wa Zanzibar Dr. Salmin Amour.

Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Dr. Salmin Amour kati kati akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania Dr. Moh’d Gharib Bilal kushoto na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi nyumbani kwake Kidombo mara baaya ya chakula cha mchana.

Hafla hiyo inayojumuisha mamia ya waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka pembe zote za Unguja huambatana pia na Maulidi ya Kuzaliwa kwa Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Duniani Mtume Muhammad { SAW  } wakati wa usiku ukiwa ni utaratibu wa  Dr. Salmin kuandaa ifikapo Mfunguo Sita wa kila mwaka.

Picha no –OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.