Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe.Samia Aanza Ziara Mkoani Geita Leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akumjulia hali mtoto Jack  Issac aliyelazwa  kwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Geita leo Januari 05, 2016 wakati alipofika hospitalini hapo kwa ajili ya kukagua hali za wagonjwa na kukabidhi Vifaa mbalimbali vya tiba.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi kifaa cha Tiba kwa mganga Mkuu wa Hospitali ya Geita Dkt. Joseph Kisala wakati alipofika hospitalini hapo kwa leo Januari 05, 2016 kwa ajili ya kukagua hali za wagonjwa na kukabidhi Vifaa vya tiba, Makamu wa Rais yupo Mkoani Geita kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi, kulshoto ni waziri wa Afya Mhe. Ummi Mwalimu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Tunzo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji wa madini GGM Terry Melpeter  kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na kampuni yake katika kusaidia maendeleo Mkoani Geita, Makamu wa Rais yupo Mkoani Geita kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua mradi wa maji safi na salama kwa wananchi wa Geita uliofadhiliwa na kampuni ya Uchimbaji madini ya GGM Mkoani humo leo Januari 05,2016, Makamu wa Rais yupo Mkoani Geita kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji madini Mkoani Geita  Terry Melpeter  wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama leo Januari 05,2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Geita kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtwisha Ndoo ya maji Bibi Veronika Lupanjo baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama Mkoani Geita leo Januari 05,2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Geita kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.