Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizung4umza na wanahabari ofisini kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala ali-pozung4umza nao ofisini kwake.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda
ya Kaskazini.
WAZIRI mkuu, Majaliwa Kassimu Majaliwa, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ibada
maalum ya kumuingiza kazini askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kiluteri
Tanzania(KKKT),Askofu Dk Frederick Shoo katika kanisa kuu la Moshi mjini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla,amesema waziri mkuu anatarajiwa
kuwasili mkoani Kilimanjaro kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro(KIA) ambapo atapokea taarifa ya mkoa kabla ya kufanya shughuli za
kanisa.
Alisema waziri mkuu hataongozana na waziri
yeyote wa serikali ya awamu ya tano bali wasaidizi wake na baada ya ziara hiyo
maalum atarejea Dodoma kuendelea na shughuli za serikali.
Ibada hiyo maalumu itajumuisha viongozi
mbalimbali wa serikali ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro sanjari na viongozi
wa madhehebu tofauti ya dini,wadau wa maendeleo,waumini na wananchi kwa ujumla.
Kutokana na ujio huo wa waziri mkuu, mkuu wa
mkoa,aliwataka wananchi hususani katika wilaya za Hai na Moshi kujitokeza kwa
wingi kumpokea kiongozi huyo ambaye pia atapokea changamoto mbalimbali
zinazoukabili mkoa
Kadhalika waziri mkuu anatarajiwa kutoa
maelekezo ya serikali kulingana na changamoto zitakazojitokeza wakati anapewa
taarifa ya mkoa.
Dk Shoo ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya
Kaskazini amechaguliwa kuongoza kanisa hilo kwa miaka minne na anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na mtangulizi wake askofu Dk Alex Malasusa ambaye amemaliza
muda wake wa uongozi.
Askofu Dk Shoo alichaguliwa mapema mwezi Agosti
mwaka jana katika mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika chuo kikuu cha
Tumaini jijini Arusha baada ya kuwashinda wenzake wawili.
Uchaguzi wa nafasi hiyo uliwashindanisha
askofu Dk Stephen Munga wa dayosisi Kaskazini Mashariki na Askofu Charles Mjema
wa dayosisi ya Pare.
Mwisho
No comments:
Post a Comment