TAARIFA KWA UMMA
UTARATIBU
WA KUPOKEA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
1.0
UTANGULIZI
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau
wakiwemo wanafunzi wa elimu ya juu kuhusu kuchelewa au kutokushughulikiwa kwa
malalamiko yao
yanayohusu mikopo ipasavyo katika ngazi za vyuo na katika ofisi za Bodi.
Kufuatia malalamiko hayo, Bodi imeboresha utaratibu wa kushughulikia maswali au
malalamiko katika ngazi zote ili kuongeza ufanisi.
Hata hivyo, kabla ya kueleza kuhusu
utaratibu huu ulioboreshwa, tungependa kueleza sifa na vigezo vinavyotoa ustahili kwa Wanafunzi kupata mkopo.
2.0
SIFA ZA
MWOMBAJI
Utoaji mikopo unaongozwa na Sheria Na. 9 ya
2004 ya Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (kama
ilivyorekebishwa) Na. 9 ya 2004 hususani vifungu vyake vya 16 na 17. Pamoja na mambo mengine, sheria hii inaitaka
Bodi kutoa msaada wa kifedha kwa njia ya mkopo kwa mwanafunzi mwenye sifa
ambaye ameomba kupewa mkopo huo umwezeshe kugharamia mahitaji yake yote au
baadhi katika masomo yake ya elimu ya juu. Hivyo basi, kila mwaka Serikali
kupitia Bodi, huandaa vigezo na sifa zitakazotumika katika kutoa mikopo kwa
mwaka husika kwa kuzingatia matakwa ya sheria. Kimsingi vigezo ambavyo
vimebainishwa na sheria ni:
a)
Awe mtanzania;
b)
Awe ameomba mkopo kupitia mtandao wa Bodi
(Online Loan and Management System (OLAMS));
c)
Awe amechaguliwa kujiunga na masomo katika
chuo chenye ithibati kinachotambuliwa na kusajiliwa na TCU au NACTE kama mwanafunzi “full time”;
d)
Awe ni mwanafunzi anayeendelea na masomo ambaye
amefaulu mitihani inayomwezesha kuendelea na mwaka unaofuata wa masomo;
e)
Asiwe ni mnufaika wa mkopo au ruzuku kutoka taasisi nyingine au watu wengine;
f)
Aliyemaliza kidato cha
sita, mafunzo ya ufundi au ualimu .....
g)
Kwa kuzingatia idadi ya
waombaji na uwezo wa Bodi ya kibajeti, mikopo hutolewa kwanza kwa:
Sheria iliyoiunda Bodi imeipa mamlaka ya kutengeneza vigezo vya nyongeza
vinavyoboresha zoezi la utoaji wa mikopo ambapo kila mwaka Bodi huandaa na
kutangaza Mwongozo wa Ukopeshaji wa mwaka unaofuatia ambao hutangazwa kabla ya
msimu wa wanafunzi kuomba mikopo kuanza. Mwongozo uliotangazwa kuongeza
uchambuaji maombi ya mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo 2015/16, ulitoa sifa
zinazowapa waombaji ustahili kama ifuatavyo:
·
Wanafunzi wanaosoma
programu za kipaumbele kwa taifa ambao hupata asilimia 100. Programu hizo ni
Sayansi za Tiba, Ualimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati, Uhandisi wa
Umwagiliaji na Uhandisi wa Gesi na mafuta;
·
Yatima;
·
Wenye ulemavu
·
Wanafunzi wanaosoma programu nyingine
hupangiwa mikopo kwa kuzingatia uchambuzi unafanywa kwa kutumia king’amuzi
uwezo (Means Testing).
3.0 UTANGAZAJI WA WAOMBAJI WALIOFANIKIWA
KUPANGIWA MIKOPO NA UANDAAJI WA MALIPO
3.1 UTANGAZAJI WA MAJINA YA WAOMBAJI
WALIOPANGIWA MIKOPO
Baada ya uchambuzi
wa taarifa zote za waombaji kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa kufanyika
taarifa za, waombaji waliofanikiwa. Kupangiwa mikopo (loan allocation) hutumwa
vyuoni, hupokelewa na Menejimenti za vyuo na kufikishwa kwenye madawati ya
mikopo (Loan Officers) ya vyuo husika huitangaza orodha hiyo kwa Wanafunzi
halali wa vyuo husika kwa njia mbalimbali kama kubandika kwenye ubao wa
matangazo (notice board) na kupeleka ofisi za Serikali za Wanafunzi.. Aidha,
orodha hiyo huwekwa kwenye mtandao wa Bodi (OLAMS) ili wanafunzi waweze kuiona.
3.2 UANDAAJI WA MALIPO
Malipo hufanywa kwa waombaji waliofanikiwa kupata Mikopo
malipo yaoo hupelekwa kwenye chuo ili
chuo kiwalipe baada ya kuwatambua vizuri kuwa ni Wanafunzi halali wa chuo hicho
kwa kuangalia vitambulisho vyao. ambapo Bodi ya Mikopo hufanya malipo kwa njia
ya ‘cheque’ kwa kukilipa chuo husika
ambacho huwajibika kuwalipa wanafunzi ndani ya siku saba (07) tangu kipokee
fedha kutoka Bodi ya Mikopo.
3.3 MAJUKUMU YA ‘LOAN OFFICER’
Mnamo mwaka 2011 serikali iliunda Tume
ambayo ilitazama namna ya kuboresha mfumo mzima wa Utoaji wa Mikopo. Pamoja na
mambo mengine, tume ilipendekeza kuanzishwa kwa madawati ya Mikopo kwenye kila
chuo. Watumishi katika madawati hayo walitakiwa kuitwa Maafisa Mikopo.
Majukumu yao yanatakiwa kuwa ni:
a.
Kutunza kumbukumbu ya
wanafunzi wote wanaopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo;
b.
Kuhakiki uwepo wa
wanafunzi waliopangiwa mikopo katika chuo chake kabla wanafunzi hao hawajapokea
malipo;
c.
Kuanzisha na kutunza
kumbukumbu ya wanafunzi wanufaika wa mikopo na wanaoacha masomo kwa sababu
mbalimbali (Kifo, uhamisho, kuahirisha n.k). Aidha, ‘Loan Officer’ huyu,
anapaswa kuandaa taarifa hizi na kuziwasilisha Bodi ya Mikopo kila mwisho wa robo
mwaka wa masomo;
d.
Kuratibu uandaaji wa matokeo ya mitihani ya
wanafunzi na kuyawasilisha Bodi ya Mikopo ndani ya siku 30 kabla ya kuanza kwa
mwaka mpya wa masomo na kwa matokeo ya marudio 9Supplimetary Examinations),
angalau siku 30 baada ya chuo kufunguliwa;
e.
Kuratibu uandaaji na uwasilishaji
wa Ankara na Madai (Invoices and Claims)
kwa wanafunzi wenye mikopo kwa ajili ya malipo;
f.
Kuhakikisha wanufaika
halali wanathibitisha upokeaji mikopo kwa kutia saini kwenye karatasi za malipo
na kuhakikisha kwa wale ambao hawajasaini, fedha zao zinarudishwa Bodi ya
Mikopo; na
g.
Kupokea na kuyafanyia
kazi maswali na malalamiko kutoka kwa wanafunzi yanayohusu utoaji wa mikopo na
kuyatolea ufafanuzi. Ikiwa yanahitaji ufafanuzi wa ziada, kuwasilisha kwa Bodi
ya Mikopo kwa hatua zaidi
4.0 UTARATIBU ULIOBORESHWA WA
KUSHUGHULIKIA MALAMAMIKO YA WANAFUNZI
Kama tulivyosema hapo awali, ili
kuboresha ufanisi wa utoaji mikopo, mwezi Agosti mwaka 2011, Serikali kupitia
iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilivielekeza vyuo vyote za elimu
ya juu kuanzisha madawati yatakayoratibu na kusimamia masuala ya mikopo na
ruzuku kwa wanafunzi wa vyuo husika. Agizo
hili limetekelezwa vizuri kiasi na hivi sasa kila chuo cha elimu ya juu kina
Afisa anayesimamia masuala ya mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wao wanaokopesheka.
Hivyo, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwakumbusha wadau wake wote, wakiwemo
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, kuhusu utaratibu wa kuwasilisha malalamiko
au maswali yanayohusu mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wa elimu ya juu kama
ifuatavyo hapa chini.
i.
KWANZA, mwanafunzi yeyote anayefadhiliwa na Serikali kupitia
Bodi ya Mikopo mwenye swali au malalamiko anatakiwa kuwasilisha suala lake kwa
Afisa mhusika anayesimamia Dawati la Mikopo/Ruzuku (Loan Officer) aliyepo chuoni
kwake. Hao ‘Loan Officers’ hivi sasa wana uzoefu wa masuala ya mikopo na ruzuku
zitolewazo na Bodi;
ii.
PILI, baada ya swali au malalamiko kupokelewa, ‘Loan Officer’
huyo anapaswa kuyapokea na kuyatafutia suluhisho malalamiko hayo na kumjibu
mwanafunzi ndani ya siku mbili (02), kama siyo siku hiyo hiyo, tangu apokee swali
au malalamiko hayo;
iii.
TATU, ikiwa siku mbili (02) zitapita bila mwanafunzi kupata
jibu, mwanafunzi awasilishe malalamiko yake kwa mamlaka ya juu ya huyo ‘Loan
Officer’ ambaye naye anapaswa kutoa majibu au kuchukua hatua ndani ya siku mbili (02), kama siyo siku
hiyo hiyo;
iv.
NNE, ikiwa kiongozi wa chuo husika cha elimu ya juu atakuwa
hana jibu la swali au malalamiko yaliyowasilishwa kwake, anapaswa kuwasilisha
suala hilo Ofisi ya Bodi ya Mikopo ya Kanda iliyo karibu na chuo chake. Ofisi
ya Kanda itawajibika kutoa jibu siku hiyo hiyo ya kupokea maswali au malalamiko
hayo au kuwasilisha suala hilo Makao Makuu ya Bodi ya Mikopo kama hana maelezo
yake;
v.
TANO, kwa vyuo vya elimu ya juu ambavyo havipo karibu na
ofisi za Kanda za Bodi ya Mikopo, uongozi wa chuo husika unapaswa kuwasiliana
na makao Makuu ya Bodi ya Mikopo moja kwa moja kwa njia ya barua pepe ifuatayo:
malalamiko@heslb.go.tz ;
vi.
SITA, baada ya kupokea malalamiko hayo, Bodi ya Mikopo Makao
Makuu itatoa majibu kwa malalamiko/maswali
yaliyowasilishwa siku hiyo hiyo au ndani ya siku mbili (02) tangu kupokelewa
kwa malalamiko au maswali hayo; na
vii.
SABA, mara tu baada ya kupokea majibu ya swali au malalamiko
yaliyowasilishwa kutoka Bodi ya Mikopo, uongozi wa chuo cha elimu ya juu utayafikisha
majibu hayo kwa mwanafunzi husika siku hiyo hiyo kupitia kwa ‘Loan Officer’ wa
chuo husika.
3.0
HITIMISHO
Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu inasisitiza kuwa ni muhimu kwa wanafunzi na wadau
wote kuzingatia utaratibu huu ili kuongeza ufanisi katika kushughulikia
malalamiko ya wanafunzi.
IMETOLEWA NA:
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
FEBRUARI,
2016
No comments:
Post a Comment