Habari za Punde


Dar es Salaam. 
Fastjet imepunguza mtiririko wa safari zake  kwenye njia ya Kilimanjaro Tanzania na Nairobi Kenya kuanzia Jumatatu Februari 15, 2016.

Fastjet ambao awali walikuwa wanatoa safari za kila siku 

kwenye njia hii hivi sasa watakuwa wanafanya  safari kutoka 

Uwanja Ndege wa  Kimataifa wa Jomo Kenyatta hadi 

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mara mbili 
kwa wiki  siku za Ijumaa na Jumapili tu.

Mabadiliko ya  mtiririko wa safari utazifanya ndege za fastjet 

kuondoka Nairobi kila Ijumaa na Jumapili saa 5.40 na kutua 

Kilimanajaro saa 6.40 na safari ya kurudi ndege itaondoka 

Kilimanjaro saa 7.10 na kutua Nairobi saa 8.10.

Kupunguzwa kwa safari hizo kumetokana na kuwepo kwa 

mahitaji kidogo miongoni mwa wateja nyakati za wiki kutoka 

masoko yote mawili ya Kilimanjaro na Nairobi na hivyo 

kufanya safari za ndege za kila siku kutokuwa nzuri 

kibiashara  kwenye siku hizo.

Shirika hilo limesema kuwa lengo lake ni kurejesha safari 

hizo kwenye njia ya Kilimanjaro –Nairobi pindi tu wateja 

wake watakapohitaji.


Safari za kila siku za  kutoka Dar es Salaam na Kilimanjaro 

hadi Nairobi zilianza Januari 11, 2016.

Mahitaji ya abiria kwa safari za ndege kwenye njia kubwa ya 

kibiashara kati ya majiji ya Dar es Salaam na Nairobi   

ambayo kwa pamoja  yana idadi ya watu zaidi ya milioni 

nane yamekuwa ni ya kuridhisha na fastjet iko kwenye mawazo kuwa  ndege moja ni lazima iongezeke kwenye safari kati ya majiji haya miwili katika siku za usoni.

Matokeo ya safari za fastjet kwenda Nairobi kutoka Dar es 

Salaam yamekuwa ni makubwa ambako kunaelezwa na 

ukweli kuwa nauli zinazotolewa na mashirika ya ushindani 

kati ya  nchi hizo mbili zimeshuka kwa  kiwango cha hadi 

asilimia 40 tangu fastjet waanze safari zake.

Nauli za fastjet kwa kiwango kikubwa zipo chini kuliko zile zinazotozwa na mashirika mengine  kwa safari za moja kwa moja kati ya Nairobi/Dar es Salaam  ambapo nauli zinaanzia dola 80 kwa safari moja.

Nauli hizo hazijumuishi kodi ya serikali ambayo ni dola 49 

kuondokea Tanzania na dola 40 kuondokea Kenya na hivyo 

fastjet kupendekeza wateja wake kufanya maandalizi 

mapema ili kutumia fursa hiyo ya tozo la nauli nafuu.

Hata hivyo fastjet inasisitiza kuwa  kupunguza safari kwenye 

njia kati ya Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa ya 

kuongeza uwezo kwenye njia za kikanda zilizopo na hali 

kadhalika uwezekano wa kuzindua  njia nyingine mpya ya 

kikanda katika siku za karibuni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.