Habari za Punde

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro Lakamata Bunduki Ikiwa Imefichwa Kwenye Tundu la Choo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Ramadhan Mungi akionesha Bunduki aoina ya Short Gun iliyokamatwa ikiwa imefichwa katika tundu la Choo katika eneo la Shirimatunda katika manispaa ya Moshi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Ramadhani Mungi akizungumza na wanahabari kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika mkoa wa Kilimanjaro hivi karibuni.


Na.Dixon.Busagaga,wa Globuu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wa watatu kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbalimbali likiwemo la mauaji pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.
Mbali na watuhumiwa hao Polisi pia imefanikiwa kukamata Bunduki aina ya shortgun (Pump Action) yenye namba 69901 ikiwa imefichwa katika tundu la choo nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa hao  eneo la Shirimatunda  katika manispaa ya Moshi.
Bunduki hiyo pamoja na risasi tatu imetajwa kukodishwa na watuhumiwa na kisha kutumika katika shughuli za kihalifu ikiwemo uporaji wa fedha katika maeneo tofauti na mali huku ikihusishwa pia kufanya mauaji.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishina msaidizi wa Polisi, Ramadhani Mungi alithibitisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na bunduki na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika.
“Katika siku za mwisho wa Desemba mwaka jana na siku za mwanzoni za mwaka huu ,kulikuwa na wimbi la matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya Short gun ambayo pia ilisababisha mauaji,tayari tumewakamata watu kadhaa na jana (juzi) asubuhi tuliweza kuikama silaha aina ya Short gun.”alisema Mungi.
Wakati huo huo matukio ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto yameendelea kushika kasi mkoani ambapo hivi karibuni mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa ) alikatwa matiti yote mawili baada ya kujinasua katika jaribio la kubakwa.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa,Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo kuwa ni Anold Josephate ambaye alitoweka na matiti hayo baada ya kuyaweka katika mfuko wa plastiki.
Alisema tukio jingine linalo ashiria kuongezeka kwa makosa ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ni tukio la juzi ambapo mwanamke mmoja aliyfahamika kwa jina la Vailet Apiniel ameuawa baada ya kunyongwa shingo.
“Siku za karibuni hapa yamejitokeza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yanayo uaibisha mkoa wetu,matukio ya ubakaji,matukio ya watu kutupa vitoto,haa ni matukio mabaya na jana tu kuna mwanaume aitwaye Denis Shayo alimnyonga mke wake”alisema Mungi.
Alisema eneo hili linahitaji kutolewa elimu ya kutosha huku akizitaka taasisi zinazojishughulisha na utetezi wa masuala ya kijinsia kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na matukio kama hayo .



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.