Mwenyekiti wa Klabu
ya waandishi wa habari Pemba Saidi Moahmed Ali, akifungua mkutano wa waandishi
wa habari juu ya ujazaji wa fomu za maombi kwa Tanzania Media Foundation,
uliofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi.
Waandishi wa habari
kisiwani Pemba, kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakimsikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa Pemba Press Club, wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku moja
ulioandaliwa na Tanzania Media Foundation
Afisa Miradi kutoka
Tanzania Media Faoundation Alex Kanyambo, akizungumza na waandishi wa habari
kisiwani Pemba juu ya TMF mpya na miradi yake kwa kipindi hiki
Mwandishi wa Habari
kutoka shirika la Utangazaji ZBC-Radio Pemba, Mchanga Haroub akiuliza swaji juu
ya uombani wa maombi kwa taasisi za kihabari
Waandishi wa habari
Radhia Abdalla wa Zenj FM na Salama Omar wa Swahiba FM, wakizungumza na Afisa
Miradi wa TMF Alex Kanyambo mara baada ya kumaliza kwa mkutano na waandishi wa
habari huko katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake
Waandishi wa habari kisiwani Pemba wakiwa katika picha ya pamoja
na watendaji wa Tanzania Media Foundation (TMF)mara baada ya kumaliza kwa
mkutano wa siku moja juu ya Ujazaji wa fomu ya maombi kwa njia ya Mtandao.
(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment