Habari za Punde

UNIDO NA CHUO KIKUU CHA MZUMBE WAENDESHA SEMINA KWA WAMILIKI WA VIWANDA VIDOGO VIDOGO VYA UZALISHAJI (SMEs) NA WAHITIMU WA VYUO TANZANIA.

Shirika la Umoja wa Mataifa  linalohusika na maendeleo ya viwanda UNIDO kwa kushirikiana na Chuo Kikuu  cha Mzumbe wameendesha semina kwa  wahitimu kutoka vyuo mbalimbali pamoja na viwanda vidogo vidogo, wafanyabiashara na  wajasiriamali wadogo wadogo Jijini Dar es salaam.


Akitoa maelezo katika semina hiyo Mkuu wa Chuo Kampasi ya Mzumbe Dar es salaam  Profesa Ganka Nyamsongoro alisema lengo kubwa la kutoa semina hiyo  ni kuwaalika vijana pamoja na wenye viwanda vidogo vigogo kujiunga katika programu  utakaoendeshwa na UNIDO kwa kushirikiana na Mzumbe.


"Lengo kubwa la programy hiyo ni kutoa  fursa kwa vijana ambao wamehitimu katika vyuo mbalimbali kuweza kufanya kazi kwa vitendo kulingana na taaluma zao pamoja na kufanya kazi na wenye viwanda vya kati na kuendesha miradi midogo midogo ili kukuza kipato chao pamoja na kuleta maendeleo kwa Taifa" alisema Profesa Nyamsongoro


Wakizungumza kwa nyakati mbalimbali wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalisjaji, wafanyabiashara na wajasiliamalia mali wamesema kuwa hii ni fursa muhimu kwao na watakuwa tayari kuwasaidia vijana hao wahitimu ambao wanategemea kuwa nao katika mafunzo ya kazi.


Kwa Upande wake Profesa Honest Ngowi ambaye ndiye msimamizi wa programu alisema UNIDO wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe watakuwa na waangalizi mbalimbali watakao zunguka kuangalia utendaji kazi wa vijana hao wakiwa kwenye programu hiyo.


Kwa upande wake ‘mentor’ wa programu hiyo Bwana Kaaya amewataka vijana wanaohitimu vyuo vikuu umuhimu wa kuweza kutumia taaluma zao katika Nyanja mbalimbali hasa kwa kutumia fursa zilizopo na kuweza kujiajiri.


Mchangiaji mwingine katika semina hiyo Bw. Deosdadit Bernard ambaye ni msimamizi wa programu hiyo kutoka UNIDO alisema programu utaendeshwa kwa muda wa miezi minne na mwishoni watakaofuzu  watapewa barua za utambulisho ili iweze kuwa rais kuajirika katika maeneo mengine kwa Urais.


Aidha mtoa mada Dr.Darleen Mutalemwa  aliwashukuru UNIDO  Chuo cha Mzumbe pamoja na kwa mchango wao katika jamii ,na amewataka wahitimu na wenye viwada vya kati na kuwataka kutokata tama na washiriki vyema katika programu hiyo kwani utatoa nafasi yaw o kuweza kuimarika katika soko la ajira.


Hata hivyo bado watu wenye viwanda vidogo vigogo vya uzalishaji na wajasiriamali pamoja na wahitimu wa vyuo vikuu wanahitajika katika kuomba nafasi ambazo bado zipo wazi kupitia katika tovuti ya www.dcc.mzumbe.ac.tz



Mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam Profesa Ganka Nyamsongoro akifungua Semina kwa ajili ya  wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara na wajasiliamali semina iliyolenga programu ya UNIDO wakishirikiana na Chuo kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kupata mafunzo ya ujuzi wa kazi.
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Peacock Hotel Dar
Mshauri wa UNIDO Bw. Mike Laizer akichangia jambo katika semina hiyo
Bw. Deosdadit Bernad Msimamizi wa Programu kutoka UNIDO akielezea kwa undani juu ya Programu  hiyo
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiendelea kufuatilia Semina
 Profesa Prosper Ngowi Msimamizi Mkuu wa Programu hiyo akieleza kwa kina nia na malengo ya wao kufanya hivyo kwa kushirikiana na 'SMEs' ili kuwapa ujuzi wa kazi wahitimu na wahitimu kutoa ujuzi wao waliokuwa nao ili kuweza kukuwa zaidi
Wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa wanaendelea kufuatilia semina hiyo kwa makini
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa wanauliza maswali na kuchangia mawazo katika Semina hiyo
Mmoja wa 'Mentor' katika programu hiyo Bw. Kaaya akiwa anatoa maelezo kwa wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali jinsi ambavyo watashirikiana katika kuwafundisha kazi wahitimu hao pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali
Picha ya Pamoja kati ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali, Chuo kikuu cha Mzumbe na wawakilishi kutoka UNIDO
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Profesa Ganka akifungua semina fupi na wahitimu kutoka vyuo mbalimbali ambao ni watanzania katika programu iliyo andaliwa na UNIDO ikiratibiwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe juu ya Mafunzo ya kazi 'Internship' ambayo yataanza hivi karibuni ambapo wahitimu hao watatakiwa kufanya kazi kwa miezi minne katika viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara  na wajasiliamali
Msimamizi Mkuu wa Programu kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Profesa Prosper Ngowi akiwaelezea wahitimu juu ya Programu hiyo
Baadhi ya wahitimu wakiwa wanauliza maswali na kutaka ufafanuzi katika baadhi ya maeneo ambayo walikuwa hawajayaelewa katika semina hiyo iliyofanyika katika Chuo kikuu cha Mzumbe
Dkt. Darleene Mutalemwa akitoa neno la Shukurani kwa wote wahitimu wote waliofika katika semina hiyo kwa niaba ya UNIDO na Chuo kikuu cha Mzumbe
Wahitimu wakiwa katika semina hiyo ya kupata maelekezo juu ya Programu ambayo inalenga kuwapa Mafunzo ya kazi wahitimu iliyo andaliwa na UNIDO ikiratibiwa na Chuo kikuu cha Mzumbe


1 comment:

  1. It was a successful meeting in Dar es Salaam. Thanks for all who attended.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.