Habari za Punde

Mradi wa PartoMa Unaoshirikisha Chuo Kikuu cha Copenhagen Nchini Denmark na Hospitali ya Mnazi Mmoja Wenye Kutowa Lengo la Ufanisi.

Dk Mohammed Hafidh akizungumza wakati hafla hiyo iliyofanyika  katika ukumbi wa Hoteli ya Tembo Forodhani, Mwenyekiti wa KMT amesema utafiti huo ambao ni wa kwanza kufanywa na kuwashirikisha watafiti wa wazalendo  Hospitali ya Mnazimmoja utasaidia kuwa na taarifa sahihi na za uhakika kwa maendeleo ya Hospitali hiyo.
Mradi wa PartoMa unaoshirikisha  Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini  Denmark na Hospitali Kuu ya Mnazimmoja  wenye lengo la kuongeza ufanisi na kuwajengea uwezo wafanyakazi  wa wodi  za wazazi katika hospitali ya Mnazimmoja umeanza kuleta mafanikio makubwa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mradi wa PartoMa kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya kiserikali Kanga Martenity Trust (KMT) iliyopo Hospitali ya  Mnazimmoja umeonyesha vifo vinavyotokana na  uzazi  na vifo vya watoto wanaozaliwa vimepungua tokea kuanza kwa mradi huo mwaka mmoja uliopita.
Akiwasilisha utafiti uliofanywa  na mradi wa PartoMa ambao uliwashirikisha madaktari, wakunga na wasaidizi wakunga katika wodi za wazazi, Dkt. Anna Maaloe amesema bado ni mapema kuthibitisha kuwa mafanikio hayo yanatokana moja kwa moja na kuwepo  mradi huo lakini ufanisi na utaalamu wa wafanyakazi  kwenye wodi za wazazi Hospitali ya Mnazimmoja umeongezeka.
Amesema Hospitali za rufaa, kama ya Mnazimmoja zinawajibu mkubwa wa kuwa na mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi waliopo na wanaotegemewa siku za mbele na kuweka miongozo bora ili kuokoa maisha ya mzazi na mtoto pamoja na wagonjwa wa kawaida.
“Kwa kuliona hilo mradi wa PartoMa umekuwa ukiandaa mafunzo  ya kuwajengea uwezo   madaktari na watendaji wa wodi za wazazi   Hospitali  Mnazimmoja siku moja kwa  miezi mitatu baada ya saa za kazi  na kuweka miongozo  ambapo  wafanyakazi wengi wamekuwa wakishiriki,” aliongeza Dkt. Anna.
Katika utafiti huo  Dkt.  Anna amesema imebainika kuwa wafanyakazi wengi wa Hospitali  ya Mnazimmoja wamehamasika kuongeza elimu na ufanisi na hiyo inasaidia katika kuokoa maisha ya  wananchi.
Hata hivyo amesema bado kunachangamoto katika kutoa huduma bora zaidi katika Hospitali ya Mnazimmoja ikiwemo  uhaba wa wafanyakazi katika wodi za wazazi ukilinganisha  na ongezeko kubwa la wazazi wanaotumia Hospitali hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hoteli ya Tembo Forodhani, Mwenyekiti wa KMT Dkt. Mohammed Hafidh amesema utafiti huo ambao ni wa kwanza kufanywa na kuwashirikisha watafiti wa wazalendo  Hospitali ya Mnazimmoja utasaidia kuwa na taarifa sahihi na za uhakika kwa maendeleo ya Hospitali hiyo.
Amesema lengo la utafiti huo ni kuwasaidia mama wajawazito kujifungua salama na kwa heshma na kuzuia vifo vya mama na mtoto ambavyo vinaweza kuzuilika.
Nae Dkt. Naufal Kassim amekiri kuwepo mtafartoMa  na ameshauri madaktari kujipanga kufanya tafiti zaidi za afya na kuyatumia  matokeo ya tafiti zilizopo kwa ukamilifu.
Katika hafla hiyo  Dkt. Ali Salum kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja aliwakabidhi  vyeti madaktari, wakunga na wasaidizi wakunga walioshiriki   mafunzo ya kuwajngea uwezo   baada ya saa za kazi  bila malipo katika hospitalihiyo. 
Dkt. Ali Salum kwa niaba ya  Mkurugenzi wa Hospitali kuu ya Mnazimmoja
akimkabidhi cheti na zawadi Metroni Mkuu wa Hospitali hiyo kwa kushiriki
 mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Mradi wa PartoMa.
Mtafiti kutoka Mradi wa PartoMa Dkt. Anna Maaloe akiwasilisha utafiti wake
 juu ya huduma za wodi za wazazi za Hospitali kuu ya Mnazimmoja.

Wauguzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja
wakimpa zawadi ya mlango na kasha Dkt. Anna  Maaloe kwa
 kazi nzuri aliyosimamia ya utafiti wa wodi za wazazi katika 
Hospitali ya Mnazimmoja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.