Habari za Punde

Naibu Waziri Mambo ya Ndani Mhe Eng Hamad Masauni Ampokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Alipofanya Ziara kutembelea Kambi ya Wakimbizi Mwisa.

Naibu Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alipotembelea Kambi ya  Utenganisho ya  Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo  inahifadhi  wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi  ya  wakimbizi kutoka nchini   Burundi kwa sababu za kiusalama.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa(kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa  Idara ya  wakimbizi,iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke. Waziri Mkuu alitembelea  Kambi ya  Utenganisho ya  Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo  inahifadhi  wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi  ya  wakimbizi kutoka nchini   Burundi kwa sababu za kiusalama.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa(kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi  Msaidizi wa  Idara ya  wakimbizi,iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Selemani Mziray. Waziri Mkuu alitembelea  Kambi ya  Utenganisho ya  Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo  inahifadhi  wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi  ya  wakimbizi kutoka nchini   Burundi kwa sababu za kiusalama.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa,akizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani), wakati alipotembelea kambi ya Utenganisho ya Mwisa iliyoko wilayani Misenyi, mkoani Kagera. kambi hiyo  inahifadhi  wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi  ya  wakimbizi kutoka nchini   Burundi kwa sababu za kiusalama.Katikati Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Mwigulu Nchemba  na kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi  Hamad Masauni.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akimuongoza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa(wa pili kulia) kwenda kuongea na wakimbizi waliohifadhiwa katika kambi ya Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera.Anayefuatia baada ya Waziri Mkuu ni Kamishna  Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja na wa mwisho ni Mkuu wa Magereza mkoa wa Kagera, SACP Omari  Mtiga. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.