Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana
na maafisa wa Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara aliyoifanya katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Katikati ni Mkuu wa wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Abuu Mvano.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana
na Maafisa wa Jeshi la Polisi, alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere kukagua shughuli zinazofanywa na Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza
na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliopo katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere na Waandishi wa Habari wakati wa ziara yake
aliyoifanya kutembelea Idara za Wizara hiyo zilizomo katika Uwanja huo.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisalimiana
na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro
alipotembelea Kituo cha Polisi Buguruni wakati wa ziara yake katika Kituo hicho.
Mkurugenzi
wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (katikati),
akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea Uwanja huo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya
Ndege, ACP Martin Otieno.
Mkuu wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere, Abuu Mvano (kulia), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kulia), alipotembelea Idara za Wizara hiyo zilizopo katika Uwanja huo.
(Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment