Habari za Punde

Rais Mstaaf wa Tanzania Al Hajj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaaf wa Zanzibar Kombandoo Salmin Amour na Mama Fatma Karume Wajumuika Wananchi Wa Zanzibar Katika Uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar Uliofanyika Leo Zanzibar.


Rais Mstaaf wa Tanzania Al Hajj Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Miembeni Skuli ya Maandalizi akipokelewa na Sheha wa Miembeni. wakati wa zoezi la upigaji wa Kura za Marudio Zanzibar uliofanyila leo Zanzibar nzima kwa Nafasi za Urais wa Zanzibar, Uwakilishi na Udiwani.  
Rais Mstaaf wa Tanzania Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akipata maelekezo baada ya kukabidhiwa Karatasi za Kupigia Kura na Karani wa Kituo cha Kupigia Kura Skuli ya Maandalizi Miembeni Jimbo la Kikwajuni.
Rais Mstaaf wea Tanzania Al Hajj Ali Hassan Mwinyi akipiga kura yake katika Kituo cha Skuli ya Maandalizi Miembezi Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Zanzibar Komando Dk Salim Amour Juma akiwasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi Jangombe Chekechea leo asubuhi kwa ajili ya kutimiza Haki yake ya Kidemokrasia ya Kumchagua Rais wa Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Zanzibar Komandoo Dk Salmin Amour Juma akiwa na msaidizi wake akipiga Kura katika Kituo cha Skuli ya Maandalizi Jongombe Chekechea. 
Mwananchi wa Shehia ya Kilimani akipiga Kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi Jangombe Chekechea Zanzibar leo asubuhi.
Mama Fatma Karume akisalimiana na Mtoto wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Slmin Amour Juma, Amini Salimin alipowasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Jimbo la Mpenda Skuli ya Maandalizi Chekechea leo asubuhi.  
Balozi Ali Abeid Karume akiwa na Mke wakiwasili katika viwanja vya Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi Jangombe Chekechea kwa ajili ya kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga Kura kumchagua Kiongozi wa Zanzibar. 
Mama Fatma Karume akiongozania na Mjukuu wake Aisha Ali Karume wakiwasili katika Kituo cha kupigiav Kura cha Skuli ya Maandalizi Jangombe Zanzibar.
Balozi Ali Karume akipokea Kura kutoka kwa Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar alipofika katika Kituo hicho Kupiga kura yake leo asubuhi.
Balozi Ali Karume akipiga Kura yake Katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi Jangombe Jimbo la Mpendae Zanzibar.
Mama Fatma Karume akitowa Kitambulisho chake cha Mpiga Kura kwa Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuhakikiwa katika Daftari la Wapiga Kura Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.