Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wa kwanza kushoto), mabati yenye thamni ya sh.milioni 200 Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa M.M.I Steel, S.K. Modi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymund Mushi na kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke,
Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (kulia), akizungumza katika makabidhiano hayo.
Wanahabari na wadau wa maendeleo wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akitoa shukurani kwa msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akitoa shukurani baada ya kupokea msaada huo.
Mwanahabri Renatus Mutabuzi wa Kituo cha Televisheni cha ITV akiwa kazini kuchukua taarifa hiyo.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano.
Na Dotto Mwaibale
UMOJA wa Viwanda vinavyoshughulika na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi nchini umemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mabati yenye thamani ya sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi msaada huo Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel alisema waliguswa mno na changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi ndio maana akawaomba wenzake wasaidie.
"Kampuni yangu imetoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 100 na Kampuni ya Ujenzi ya Estim imetoa sh.milioni 50 wakati Export Trading imetoa sh. milioni 50" alisema Patel.
Patel alitumia fursa hiyo kuyaomba makampuni mengine kujitoa kusaidia shughuli za maendeleo nchini hasa katika sekta ya elimu yenye changamoto za uhaba wa madarasa na madawati.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya madarasa jijini Dar es Salaam hasa katika Wilaya ya Temeke na Ilala ambapo katika shule moja kuna zaidi ya wanafunzi kuanzia 3000 hadi 5000.
Sadiki alisema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto hiyo katika jiji la Dar es Salaam.
Hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, Ilala, Raymond Mushi na Mkurugenzi wake.
No comments:
Post a Comment