Habari za Punde

Wanafunzi wa Skuli za Unguja na Wananchi wa Jimbo la Chaani Watembelea Baraza la Wawakilishi Chukwani.

Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Wilaya ya Kaskazini Unguja Mhe. Nadir Abdullatif, akizungumza na Wananchi wa Jimbo lake waliofika katika jengo la Baraza la Wawakilishi kujionea shughuli za Mkutano wa Baraza zinavyondelea kwa michango ya Wajumbe wakiwa nje ya jengo hilo. 

Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar akiwatembeza Wananchi wa jimbo lake katika jengo la baraza la wawakilishi walipofika kutembelea na kujionea shughuli za Baraza zinavyoendesha. 

Wanafunzi wa Skuli za Unguja wakitembelea Baraza la Wawakilishi Zanzibar kujionea shughuli zinazofanywa katika Jengo hilo wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kitengo cha Chumba cha Hansad, wakati Mkutano wa Baraza ukiendelea, Wakiwa katika ziara ya kimasomo kutembelea Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.