Mkuu
wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa
mtandao unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akisisitiza jambo wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa mtandao
unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kushoto Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel
upande wa Zanzibar, Ibrahim Attas.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akisisitiza jambo wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa mtandao
unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kulia ni Mkuu wa Zantel upande wa
Zanzibar, Mohamed Mussa, na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel
upande wa Zanzibar, Ibrahim Attas.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Mkuu wa Zantel.
Kampuni ya simu inayoongoza visiwani Zanzibar, Zantel, imewekeza jumla
ya dola milioni 10 za kimarekani ili kuimarisha huduma zake za mawasiliano
nchini.
Mpango huo unajumuisha kubadilisha mfumo mzima wa mawasiliano kwa
kubadilisha vifaa vilivyokuwepo na kuweka mitambo mipya kwa madhumuni ya
kuimarisha mawasiliano ya simu na kuongeza kasi ya mtandao.
Akizungumza na waandishi
wa habari visiwani humu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Bwana Benoit Janin
alisema kuimarisha huko katika huduma za simu na mtandao kwa upande wa Zanzibar
ndio kilikuwa kipaumbele cha kwanza cha kampuni ya Zantel.
‘Kampuni ya Zantel
imeanza safari mpya kabisa yenye lengo la kuimarisha na kurudisha nafasi ya
mtandao wa Zantel katika ubunifu na kutoa huduma bora visiwani hapa’ alisema
bwana Janin.
Bwana Janin pia alisema
uboreshaji wa huduma za Zantel ni mpango endelevu na katika kipindi kifupi
kijacho, Zantel itaendelea kufunga vifaa vipya hali ambayo itawafanya wateja
waweze kuwasiliana kwa bei nafuu na bila ya bughudha.
‘Maboresho haya
yamelenga kuhakikisha tunakuza na kuimarisha teknolojia ya mawasiliano ikiwa ni
pamoja na kutoa huduma za kipekee na kutekeleza ahadi yetu ya kuendelea
kuongoza katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu’ alisema Bwana Benoit.
Janin pia alielezea
mpango wa kampuni ya Zantel kuboresha huduma ya EzyPesa kwa kurekebisha mfumo
mzima ili uweze kuhimili mawakala wengi na kuongeza huduma za ndani ya mfumo
huo.
Katika kipindi kifupi pia kampuni ya Zantel pia imefanikiwa kuondoa
mtandao wa 2G na kuweka mtandao wa 3G, sambamba na kuzindua rasmi mtandao wa
kasi wa intaneti wa 4G mjini Unguja.
‘Nina furaha kubwa jinsi
utekelezaji wa mikakati yetu unavyoendelea wa kuboresha huduma zetu ambao utawapa
wateja wetu nafasi ya kufurahia huduma zetu na pia kuwapunguzia gharama za
mawasliano huku tukukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa wakati huu na siku zijazo’
alisema Janin.
Bwana Janin pia alisema tayari matatizo ya
mawasiliano ya huduma za 3G yameshatatuliwa kwa kutumia mkonga wa fiber katika
ya maeneo ya Unguja na Pemba.
‘Tumefanikiwa kuyatatua
matatizo madogo madogo katika mji mkongwe kwa kuweka vifaa ambavyo vimesaidia
sana kuondoa msongamano wa mawasiliano majumbani na katika sehemu za wazi’
alisema Janin.
Kampuni ya Zantel ambayo
ilizindua huduma ya mtandao wa 4G katika mji wa Unguja mwezi uliopita pia
imefanikiwa kufikisha mawasiliano kwa asilimia 80% ya watanzania kutoka
asilimia 40% waliyokua wanawafikia awali.
No comments:
Post a Comment