Habari za Punde

Apelekwa rumande kwa Ubakaji.

Na Haji Nassor, Pemba
Mahakama ya Wilaya Chakechake, imelazimika kumfutarisha rumande kijana Hamad Khamis Juma (36), mkaazi wa Mtambwe, kwa muda wa wiki mbili, akikabiliwa na tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka (13) ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
Mahakama hiyo chini ya hakimu wake Omar Mcha Hamza na mwendesha mashitika Seif Mohamed Khamis, mara baada ya kusomewa tuhuma hiyo, hakutakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.
Hakim Omar Mcha, alimwambia mtuhumiwa huyo aende rumade hadi Juni 21, mwaka huu, na atakaporudi atakutana na hakimu wake wa mahakama ya Mkoa, ambayo kisheria ndio yenye mamlaka ya kusikiliza shauri kama hilo.
Hati ya mashitaka iliosomewa mahakamani hapo, na mwendesha mashitaka Seif Mohamed ilidaa kuwa mtuhumiwa huyo, alimbaka mtoto huyo eneo la Sompia Chakechake na kumsababishia maumivu.


“Unadaiwa kumbaka mtoto mdogo, Juni 9, mwaka huu na kumsababishia maumivu makali, jambo ambalo ni kosa kinyume na kifungu cha 125 (1) na (2) (e) na kifungu 126 (1) sheria ya namba 6 ya mwaka 2004, sheria ya Serikali Zanzibar’’,alidai mwendesha mashitaka.
Kwa vile mtuhumiwa huyo hakutakiwa kujibu chochote, lakini alidai kulalamikia kuitaka mahakama hiyo impe dhamana kutokana na kujihisi maumivu makali mwilini mwake, baada ya kupigwa na watu wenye hasira.
“Muheshimiwa naomba dhamana, maana hali yangu taabani, unajua juzi nilipokutikana na mtoto huyo, watu walinipiga sasa najihisi maumivu’’,alilalamika kwa sauti ndogo mahakamani hapo.
Hata hivyo maelezo ya mtuhumiwa huyo wa ubakaji, hayakuzingatiwa na hakim Omar Mcha, akisema hana mamlaka ya kumsikiliza wala kumpa dhamana kisheria.


Mthumiwa huyo amelazimika kwenda rumande hadi Juni 21, mwaka huu, ambapo kesi yake itaendelea chini ya mahakama ya mkoa, ambayo ndio kisheria ndio nyenye mamlaka ya kusikiliza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.