Habari za Punde

Hafla ya Uwashaji Mwenge wa Mashujaa Mkoani Dodoma Jana Usiku.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Solomon Mndeme (katikati) akiuwasha mwenge wa Mnara wa kumbukumbu ya mashujaa saa sita za usiku wa tr 25julai 2016 kama ishara ya Uzinduzi wa mnara huo   kuwakumbuka ya mashujaa uliopo  katika viwanja vya Mnara wa mashujaa Mjini Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Solomon Mndeme (katikati) na Viongozi wengine akiwepo Waziri wa Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe,Jenista Mhagama wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa  baada ya kuwashwa mwenge wa Mnara wa kumbukumbu ya mashujaa saa sita za usiku wa tr 25julai 2016 ikiwa ni ishara ya uzinduzi waa mnara wa  kumbukumbu ya mnara wa  mashujaa uliopo katika  viwanja vya Mnara wa mashujaa Mjini Dodoma
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maadhimisho ya uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya mashujaa wakishudia uwashwaji mwenge katika viwanja vya Mnara wa mashujaa Mjini Dodoma  uliowashwa na  Mkuu wa Wilaya Dodoma Mhe, Christina Solomon Mndeme,usiku wa saa sita kamili jana
Waziri wa Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe,Jenista Mhagama na Mkuu wa   Mkoa Dodoma Mhe,Jordan Mungire Rugimbana (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa mbele ya mnara wa mashujaa katika hafla ya uzinduzi wa mnara huo yaliyofanyika jana,
Mkuu wa   Mkoa Dodoma Mhe,Jordan Mungire Rugimbana alipokuwa akizungumza machache na kumkaribisha Waziri wa Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe,Jenista Mhagama kutoa hutuba yake kwa Viongozi wengine na wanakamati wa maadhimisho ya kumbukumbu za mashujaa katika hafla ya uzinduzi wa mnara kwa uwashawaji wa Mwenge  uliyofanyika jana usiku.
Waziri wa Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe,Jenista Mhagama akitoa hutuba yake kwa Viongozi  na wanakamati katika hafla  ya uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu ya mashujaa katika hafla ya uzinduzi uliyofanyika jana Mjini Dodoma (kushoto) Mkuu wa   Mkoa Dodoma Mhe,Jordan Mungire Rugimbana
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maadhimisho ya Siku ya mashujaa na Viongozi wengine wakimsikiliza Waziri wa Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe,Jenista Mhagama akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Mnara kwa uwashwaji Mnara wa Kumbukumbu ya mashujaa saa sita za usiku Mjini Dodoma
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakipiga wimbo wa Taifa baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa Mnara  wa Kumbukumbu ya mashujaa kwa kuwashwa mnara huo jana saa sita za usiku Mjini Dodoma.24/07/2016. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.