Habari za Punde

Jeshi la Polisi Mbeya Lamshikilia Baba Mzazi wa Kijana Aliefungwiwa Ndani Miaka 11.

 Baba Mzazi wa kijana Emanuel Fedrick (20) mwenye tatizo la akili na viungo , aliyejitambulisha kwa majina ya Fedrick John Mkazi wa Mwambenja Iganjo Mbeya ,ambaye anadaiwa kumfungia ndani mtoto wake kwa zaidi ya miaka 11 bila kumpatia matunzo yoyotte katika kipindi chote hicho.
Kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambeenja kata ya Iganzo mwnye tatizo la akili na mwili akiwa amelala kitandani kwa zazidi ya miaka 11 sasa kutokona na ulemavu wake wa akili na viungo huku  wazaziwake wakishindwa kumlea vyema na kumpa huduma bora kama walivyo watoto wengine.

Kijana EmanueL Fedrick (20) wenye tatizo la akili akiwa amepaktwa na shangazi yake Stella John mara baada kumaliza kupatiwa chakula.


Na EmanuelMadafa,JamiiMojablog-Mbeya
JESHI la Polisi kupitia dawati la jinsia na watoto linamshikilia Baba mzazi wa  kijana mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na akili ,Emanuel Fedrick iambaye alifungiwa ndani  kwa zaidi ya miaka 11 na wazazi wake.
  
Kijana huyo, mwenye umri wa miaka 20, Fredrick Emmanuel  Mkazi wa Mwambeja Kata ya Iganjo jijini hapa amekuwa akiishi ndani bila ya kutolewa nje kwa kipindi cha miaka 11, hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa kudhohofisha mwili wa kijana huyo kiafya.
             
Tukio la kukamatwa kwa mzazi huyo limetokea Julai 14 ,2015 majira ya asubuhi nyumbani kwakwe katika eneo la Mwambenja Kata ya Ilemi lililopo Jijini hapa.
  
 Akizungumzia hilo, Mkuu wa dawati la jinsia Mkoa wa Mbeya, Afisa wa Polisi Janet Masangano, amesema baba mzazi wa kijana huyo Emmanuel John, anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano kufuatia tuhuma zinazomkabili za kumficha mtoto ndani kwa zaidi ya miaka 11 hali ambayo imetafsiliwa kuwa ni ukatili wa kijinsia kwa motto huyo.
  
Amesema, sheria ya mtoto ilipitishwa na serikali mwaka wa 2009, sheria hiyo huwalinda watoto dhidi ya mazingira hatarishi na unyanyasaji na kwamba Kama kila mtu mzima akilea mtoto mmoja, watoto (wote) wa Tanzania watakuwa katika mazingira salama.

Amefafanua kuwa , maelezo ya awali ya wazazi wa kijana huyo, yameweka bayana kwamba walezi hao baada ya kumuhangaikia kwa muda mrefu ya bila kupata nafuu, sasa wameamua kumtelekeza kijana huyo na  kuamua kumfungia ndani na kumuachia mungu kama walivyoeleza.

Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa mtaa wa Mwambenja, Rosemary Jama, amesema taarifa za Ferdrick kuishi ndani ya nyumba hiyo  walikuwa nazo lakini hawakuwahi kupata taarifa za kwamba kijana huyo hatolewi nje.

Kugundulika kwa kijana huyo kunatokana na taarifa zilizotolewa na mmoja wa wanafamilia ambaye hakupendezwa namna kijana  huyo anavyo hudumiwa na wazazi wa mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.