Habari za Punde

Maadhimisho ya tamasha la mzanzibari kisiwani Pemba


Ngoma maarufu ya Utamaduni  ya Msondo ambayo kwa sasa imepotea Kisiwani Pemba, ikichezwa na akinamama wa Kijiji cha Kangagani  Mkoa wa Kaskazini Pemba, ili kutia hamasa katika mchezo wa Ng'ombe uliofanyika katika Kiwanja cha Kangagani Skuli, katika maadhimisho ya Tamasha la Mzanzibar.
Mchezaji wa  Ng'ombe maarufu , Abdalla Seif, akipata kipigo kutoka kwa Ng'ombe aliejuilikana kwa jina la Shika lako, baada ya kutofanikiwa kumpiga chenga(ngea) hukoa katika viwanja vya Kangagani Kisiwani Pemba, katika shamra shamra za Tamasha la Mzanzibar.
Ng'ombe aliejuilikana kwa jina la Msamba, akitowa kipigo kwa miongoni mwa Wachezaji wa mchezo huo huko katika kiwanja cha Kangagani Kisiwani Pemba, katika shamra shamra za Tamasha la Mzanzibar.
Katibu Tawala wa mkoa wa Kaskazini Pemba,Yussuf Moh'd Ali , akiwamgeni rasmi wa Tamasha hilo akizungumza  jambo kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa Ng'ombe huko Kangagani Pemba.
Baadhi ya viongozi mbali mbali wakiongozwa na Ofisa mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Khatib Juma Mjaja, wakimsikiliza kwa makini Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yussuf Moh'd Ali , huko katika Kiwanja cha Kangagani  katika shamra shamra za Tamasha la Mzanzibar.


Ng'ombe aliejuilikana kwa jina la Pua mbovu, akimkosa mchezaji wa mchezo huo baada ya kufanikiwa  kumpiga chenga (Ngea).


Baadhi ya Wananchi wa Kisiwa cha Pemba, wakiangalia Mchezo wa Ng'ombe ambao ni maarufu sana Kisiwani humo,pamoja na kwamba umeanza kupotea na kuchezwa kwa nadra katika sherehe kama hizi tafauti na hapo mwanzo ambapo ulikuwa unachezwa kila baada ya mavuno ama sherehe mbali mbali za kitaifa.

Picha zote na Bakar Mussa-Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.