Habari za Punde

Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) Yazindua Usajili kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Kujiunga na NHIF

Afisa Habari wa NHIF Ndg. Singo akitowa maelezo wakati wa Uzinduzi wa Usajili kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya NHIF hafla hiyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa Baraza Chukwani Zanzibar.  
Meneja wa NHIF Tawi la Zanzibar Ndg Ismail Kangeta akizungumza wakati wa uzinduzi wa usajili kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliozinduliwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg Raya Mselema akizungumza wakati wa Uzinduzi huo wa kujiunga na Bima ya Afya kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi mdogo wa baraza chukwani Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Ndg. Bernard H Konga, akizungumza wakati wa uzinduzi huo na kutoa maelezo ya Bima ya Afya faida zake kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa Uzinduzi wake uliofanywa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akizundua Usajili wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF ) Uzinduzi huo umefanyika katika jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar ukumbi mdogo wa baraza Chukwani. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.