Habari za Punde

Moto katika Soko la Mwanakwerekwe Unguja Lasababisha Hasara kwa Wafanyabiashara katika Eneo la Mabanda ya Mitumba.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar wakiwa katika zoezi la kuzima Moto uliotokea katika Soko la Mwanakwerekwe Zanzibar na kusababisha hasara  za mali za Wafanyabiashara katika Soko hilo kutokana na moto huo uliosababisha kuunguza bidhaa katika eneo hilo lililokuwa na wafanyabiashara wa miotumba na mama lishe. Wananchi walioshuhudia  janga hilo wanasema moto huo umesababishwa na jaa lilioko karibu na soko hilo moto huo ulikuwa ukiwaka kila siku kutokana taka zilizokuwepo hapo siku ya tukio kulikuwa na upepo mkubwa uliosababisha kurukia katika mabanda hayo. 
Sehemu ya mabanda yalioharibika na moto huo ya biashara za mitumba katika soko hilo la mwanakwerekwe Unguja.
Wananchi na Wafanyabiashara wakiwa katika eneo hilo la tukio wakiwa na huzuni kwa kuharibika kwa mali zao na kupata hasara kubwa. 

Wananchi wakiangalia jinsi ya Moto ukiteketeza baadhi ya mabanda ya Wafanya Biashara katika Soko hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.