Habari za Punde

Naibu Waziri wa Habari Mhe Chuom Afufua Matumaini.

Na Haji Nassor, Pemba
UONGOZI wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar umefufua matumaini na dira mpya kwa wafanyakazi wa wizara hiyo, ukisemka uko tayari kushirikiana ili kutimiza malengo yaliopo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa wizara hiyo Zanzibar Mhe: Chuom Kombo Khamis na Afisa Mdhamini Pemba Khatib Juma Mjaja, wakati wakizungumza na watendaji wakuu wa wizara hiyo kisiwani Pemba.
Naibu Wiziri alisema, ingawa kwa sasa bado ni mapema kusema watamaliza changamoto zote kwa haraka, lakini malengo na dhamiri yao, ni kuhakikisha utulivu ndani ya kazi unapatikana.
Mhe: Chuom alisema kuwa, anachohitaji kutoka kwa wafanyakazi, ni umoja na ushirikiano wa dhati wakati wote wa utendaji wa kazi, ili kila mmoja atekeleze wajibu wake ipasavyo.

“Jamani sisi ndani ya wizara hii ni wapya, lakini tumedhamira hasa, kuona tunafikia malengo ya wizara yetu, lakini lazima kila mmoja awajibike’’,alifafanua.
Katika hatua nyengine Naibu waziri huyo wa wizara ya Habari, amewakumbusha wafanyakazi, kutozitumia ofisi kama majukwaa ya kisiasa, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria.
Nae Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Kisiwani Pemba Khatib Juma Mjaja, alisema lengo hasa baada ya kipindi kifupi ni kuona wakuu wengine wa taasisi za kiserikali wanaiga mfano wa utendaji wa wizara hiyo.
Alisema anaelewa vyema changamoto zilizomo ndani ya wizara hiyo na hasa kwa vile amelelewa na kufanyakazi kwa muda mrefu, sasa kazi yake ni nyepesi kwa kuwataka watendaji wakubali madiliko.
“Jamani tukubalini na sasa kama alivyosema Mhe: Rais wetu tusifanye kazi kwa mazoea, na mini naamini tukifanya hivyo tutafika mbali’’,alifafanua.
Baadhi ya wakuu wa Idara zilizomo ndani ya wizara hiyo kisiwani Pemba, walisema wameshachoka kuzizungumza changamoto zinazowakumba, ingawa wanamatumaini makubwa na safu mpya.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Marzuk Khamis Sharif, alisema wanakabiliwa na changamoto ya usafiri kwa muda mrefu, na kuwa na ufinyu wa kusambaaza habari.
Aidha fundi za ZBC Redio Abdalla Abeid, alisema uchakavu wa baadhi ya mashine na mitambo, husababisha redio hiyo kuwa na usikivu hafifu kisiwani Pemba.

Ziara hiyo na Naibu waziri wa wizara ya habari Mhe: Chumo Kombo Khamis pamoja na kikao cha Afisa mdhamini Pemba Khatib Juma Mjaja ni chakwanza tokea walipoteuliwa wiki mbili zilizopita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.