Habari za Punde

Ndugu na jamaa wa Marehemu Abubakar Ibrahim Sumari wanatafutwa

Picha inayoonekana ni Marehemu Abubakar Ibrahim Sumari alikuwa anaishi Mkunazini Zanzibar na ameonekana na kadi ya CUF yenye jina hilo ameichukulia Makao makuu ya CUF Mtendeni. 

Naomba mnisaidie kuwatafuta jamaazake. Maiti imehifadhiwa MORTUARY katika Hospitali ya Wilaya Korogwe (Magunga) .

Namba yangu ni 0777423770 au 0673423770. 

Au wasiliana moja kwa moja ktk vyombo husika Korogwe. Marehem amefariki njiani katika safari huko Mombo Mkoa wa Tanga na anaonekana alikua anaugua Pumu kwakua amekutikana na vidonge vya kutibu PUMU. Hii ni picha yake iliomo ktk kadi ya uanachana wa chama na picha ya kadi yenyewe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.