Habari za Punde

Sala ya Idd el Fitr kusaliwa viwanja vya Maisara, Baraza litafanyika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI            

Kamati ya Taifa ya Sala na Baraza la Idd inatangaza kuwa sala ya Iddi el Fitri Kitaifa itasaliwa katika Kiwanja cha Maisara saa 1.30 asubihi kesho ikiwa mwezi utaonekana leo jioni, iwapo kutanyesha mvua sala itasaliwa katika Msikiti wa Mwembeshauri.

Baraza la Iddi litafanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni kuanzia saa 3.30 asubuhi watakaopata mwaliko wanatakiwa wawe wameshakaa katika ukumbi saa 3.00 kamili asubuhi.

Tunawatakia Siku kuu njema.   

IDDI MUBARAK.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.