Habari za Punde

Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar Likiendelea na Maonesho Yake Ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar.


 Kikundi cha Yausi Zanzibar kikisoma Maulid ya Home wakati wa Maonesho ya Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar (ZIFF) linalifanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe katika Nji Mkongwe wa Zanzibar likiendelea na Maonesho yake.


 Maonesho ya Filamu mbalimbali zikioneshwa katika Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar katika ukumbi wa Ngombe Kongwe Zanzibar moja ya Filamu ya Mtunzi kutoka Ujerumani inayozungumzia Utukutu wa watoto wadago wakiwa chini ya umri wa miaka 14,
 Mtunzi wa Filamu hiyo kutoka Nchini Ujerumani Viet Helmer akiwa na Vijana wa Tamasha la ZIFF wakifuatilia filamu hiyo wakati ikioneshwa katika Tamasha hilo la ZIFF Zanzibar.
 Watoto wakifuatilia filami hiyo katika viwanja vya ngome kongwe Zanzibar.
 Mkurugenzi wa ZIFF Martin Mhando akitowa tafsiri ya maelezo ya filamu hiyo wakati ikitolewa maelezo yake na mtunzi wake Veit Helmer baada ya kumalizika kuoneshwa. 
 Washereheshaji wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF wakitowa maelezo katika Ukumbi wa Mambo Club Ngome Kongwe wakati wa Tamasha hilo wakijulisha vikundi vya Burudani kwa wananchi waliohudhuria Tamasha hilo. Kikundi cha Dance cha Unit Six kikitowa burudani katika Jukwaa la Tamasha la Nchi za Jahazi katika Ukumbi wa Mambo Club Ngome Kongwe Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.