Habari za Punde

Tigo, serikali zasaini makubaliano kuunganisha shule za sekondari na intaneti


Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka Tigo, Shavkat Berdiev® na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora(L) wakisaini makubaliano kwa ajili ya kuunganisha kufikiwa kwa intaneti katika shule za sekondari nchini ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni katika hafla iliyofanyika mapema jana katika shule ya sekondari Jangwani Jijini Dar es salaam.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora akiongea na mmoja wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani mara baada ya kusaini saini makubaliano kwa ajili ya kuunganisha kufikiwa kwa intaneti katika shule za sekondari nchini ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni katika hafla iliyofanyika shuleni hapo mapema jana.


Dar es Salaam  Julai 13, 2016-kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imeingia ubia na Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha kufikiwa kwa intaneti katika shule za sekondari nchini  ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni  katika zoezi ambalo litachukua miaka miwili.


Kama sehemu ya makubaliano hayo, wizara itabainisha na 

kutoa orodha ya  shule zisizo na maabara za kompyuta ili 

ziunganishwe na hali kadhalika  kuongoza utekelezaji wa 

mradi  wakati Tigo itadhamini maendeleo ya miundombinu 

katika shule nchini ikiwa ni pamoja na kuunganisha nyaya 

ndani ya madarasa  na kufunga visivyotumia nyaya (LAN) 

na vituo vinavyofikia  mtandao wa intaneti.



Alipokuwa akisaini makubaliano hayo katika Shule ya 

Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa 

Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev, alisema, “Kupitia Idara 

yetu ya huduma kwa jamii hivi sasa tunatekeleza  dira ya 

serikali  ya kuibadilisha nchi kuingia katika uchumi 

uliojikita katika uelewa ifikapo mwaka 2025 na kampuni 

yetu  imejipanga kuhakikisha  shule nyingi za sekondari 

Tanzania  zinafikiwa na mtandao wa intaneti.

“Tunajivunia  kushirikiana na Wizara ya mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu  katika kuwezesha vijana  na jamii kwa ujumla  kuingia katika  mkondo wa kidunia wa habari  na uelewa, ambako watajifunza, kupanua uelewa wao na kushirikiana na wenzao katika sehemu mbalimbali duniani.”

Berdiev aliongeza kusema, “Tigo itaendelea  kufanya kazi 

na serikali  katika miradi  mingine ya ubunifu na inayovutia ili kunyanyua maisha ya Watanzania walio wengi”.

Akiishukuru Tigo wakati wa kusaini makubaliano hayo 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na 

Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora alisema, “Ni kupitia 

ushirikiano kama huu ndipo tutaweza kusambaza stadi za 

kisasa za Tehama pamoja na uelewa kwa vijana ili 

kuwawezesha  kukabiliana na changamoto  zinazotokana na 

mtiririko wa mabadiliko ya habari ya kila siku ndani ya 

jamii na katika uchumi wa dunia.”

Prof. Kamuzora aliongeza, “Naipongeza Tigo kwa utayari 

wake wa kujingiza katika makubaliano baina ya sekta 

binafasi na sekta za umma ili kuwasaidia wanafunzi wa 

shule za sekondari nchini Tanzania na vile vile 

tunakaribisha wadau wengine  kushiriki kuunganishwa kwa 

teknolojia hii.

Mradi wa kielektroniki mashuleni (eSchools) ni moja ya miradi mkakati ya uwekezaji kijamii ya Tigo na hadi sasa Tigo imeweza kuunganisha shule 31 za sekondari za serikali  na  mtandao wa intaneti ikiwa na mpango wa baadaye wa kuziunganisha  shule 50 kwa mwaka huu.

1 comment:

  1. Sasa hapa ndo tutaona raha ya kutegemea cha ndugu, (labda watu ones huruma)ila hio sio ya muungano,sie tulikuwa na shirika letu la ubia na linaizwa kwa dola moja tu kwa hao tigo, sasa hatukujua kuwa baadae tutakuja kuhitaji mtandao kwa matumizi ya serikali, hospital na shule ? Je tungelinunua na kuwa Mali yetu si tungeweza kupata kuunganisha bure ? Maana lile shirika lilikuwa linamiliki hisa kwenye mkonga wa baharini (Afrika kusini mpaka Jibuti), na pia wana dish pale amani, ila serikali haina vision za mbali, hao tigo sijui kama hawatoliuza kwa mtu mwengine ilhali sisi tungekuwa tunalimiliki, hao SMT wamelikwamua Lao kutoka kwa airtel, ila sisi ....Mola atustiri na kukusaidia.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.