Habari za Punde

Wajumbe wa Halmashauri Kuu Wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano White House Dodoma.

Wajumbe wa Mkutano wa Halmaashauri Kuu ya CCM wakiwa katika ukumbi wa mkutano jengo la CCM White House Mkoani Dodoma, wakisubiri Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika ukumbi na kuufungua mkutano huo kupitisha jina la Mgombea Nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk John Pombe Magufuli. kuchukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti kujiuzulu na kufanyika Mkutano Maalum wa kumchagua Dk Magufuli kuchukua nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kesho katika Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi huo Mjini Dodoma.
Wajumbe wakibadilisha mawazo wakiwa ukumbi wa mkutano wakimsubiri Mwenyekiti kuufungua mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya CCM, uliofanyika katika Jengo la White House Mjini Dodoma leo asubuhi. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Karume akizungumza na Waziri Mkuu Mstaaf Dk Salim Ahmeid Salim wakati wa mkutano huo mjini dodoma.
Balozi Ali Karume akisisitiza jambo wakati akizungumza na Balozi Ali Mchumo wakiwa katika ukumbi wa mkutano kabla ya kuaza kwake.
Wajumbe wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakibadilishani mawazo kabla ya kuaza kwa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Borafya Silima,akisalimiana na Wajumbe wakati akiingia katika ukumbi wa mkutano.
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wakipitia makabrasha yao kusoma ajenda za mkutano huo.
Waheshimiwa  wa Halmashauri Kuu ya CCM wakizungumza kabla ya kuaza kwa mkutano huo leo sabuhi katika jengo la CCM White House Dodoma. 
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wakibadilishana mawazo wakati wakiwa katika ukumbi wa mkutano white house mjini dodoma leo.
 Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwa katika ukumbi wa mkutano kabla ya kuaza kwa mkutano huo uliofunguliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwa wamesimama wakati Viongozi wa Kitaifa wakiingia katika ukumbi wa mkutano.
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwa katika ukumbi wa mkutani wakisubiri ufunguzi wa mkutano huo kupitisha jina la mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana akizungumza wakati wa mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete kuufungua mkutano huo. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa CCM jengo la white house mjini dodoma leo asubuhi, kulia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na kushoto Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa CCM jengo la white house mjini dodoma leo asubuhi, kulia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, na kushoto Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.