Habari za Punde

Wakaazi wa Zanzibar wanufaika na kapu la Vodacom Foundation

 Mkazi wa Masingini Zanzibar,Mzee Mtumwa Haji Mustafa (kulia) akipokea kapu lenye vyakula mbalimbali kutoka kwa mwakilishi wa Doris Mollel Foundation, Warda Walid(kushoto)na Meneja mauzo wa kanda hiyo wa Vodacom Tanzania, Mohamed Mansour(katikati)ikiwa ni msaada kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation.
 Meneja mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Zanzibar, Mohamed Mansour(kushoto) na mwakilishi wa Doris Mollel Foundation, Warda Walid (kulia) wakimkabidhi kapu lenye vyakula mbalimbali Bi.Mwamvua Makame mkazi wa mji huo, ikiwa ni msaada uliotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mkazi wa shehia mahameni mjini Zanzibar, Bi.Mwajuma Juma(katikati) akipokea kapu lenye vyakula mbalimbali kutoka kwa Meneja mauzo wa kanda hiyo wa Vodacom Tanzania, Mohamed Mansour(kulia)ikiwa ni msaada kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation ,kushoto ni mwakilishi wa Doris Mollel Foundation, Warda Walid.

1 comment:

  1. Vizuri kusaidia watu wakati wowote sio lazima mwezi huu wa ramadhan , lkn haifai na sio vizuri kujitangaza na kuwatangaza watu unaowapa

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.