Habari za Punde

Watendaji wa ZSTC Watakiwa Kufanya Kazi kwa Bidii Kuimarisha Zao la Karafuu Kisiwani Pemba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC)  Dk, Said Seif  Mzee, akizungumza na baadhi ya Watendaji wakuu wa Shirika hilo Kisiwani Pemba, huko katika ukumbi wa Kiwanda cha mafuta ya Makonyo

Wawi Kisiwani humo.

Baadhi ya Watendaji wa ZSTC Zanzibar, wakimskiliza kwa makini Mkurugenzi wa shirika hilo huko katika Kiwanja cha mafuta ya makonyo Wawi Pemba.
Karafuu zikiwa zimeanikwa huko katika kituo cha ununuzi cha Madungu Chake Chake Pemba, zikiwa zimeanikwa ili ziweze kukauka vyema na hatimae kuweza kununuliwa na Shirika la ZSTC.

Mkurugenzi Utawala wa shirika la Biashara la Taifa Zanzibar(ZSTC) Ussi Moh'd Juma, akiangalia Karafuu ambazo zilikuwa zimeanikwa huko katika kituo cha ZSTC Madungu ambazo wanunuzi walikataa kuzinunuwa hadi pale zitakapokauka vyema.(Picha na Bakar Mussa -Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.