Habari za Punde

Wazee Zanzibar watoa Shukrani na Pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar, Dk Shein

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya Wazee ambao wametimiza miaka 70 ambao wanapokea mafao maalum ya uzeeni yaliyoidhinishwa na Rais wakati alipofika katika Viwanja vya Wazee Sebleni kwa ajili ya kumshukuru na Kumpongeza leo,[Picha na Ikulu.] 12/07/2016.
  Wazee waliostaaafu katika Idara mbali mbaliu za Serikali na ambao wametimiza Umri wa miaka 70 wakiwa katika viwanja vya Makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja wakati wa Shukurani maalum za Wazee hao na kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuwawezesha kupata mafao katika umri huo,hafla iliyofanyika leo,[Picha na Ikulu.] 12/07/2016.
 Wazee wa Wilaya ya Kusini Unguja nao walihudhuria katika hafla ya kumponheza na kumshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuwawezesha kupata mafao ya kufikia umri wa miaka 70 katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 12/07/2016.
 Msoma utenzi Bw.Mohamed Abdalla Zungu kutoka Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akighani Utenzi wake wakati wa hafla ya Shukrani na Pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein zilizotolewa leo na Wazee wanaopokea pencheni kwa kutimiza umri wa miaka 70 katika Viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 12/07/2016.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mzee Bi Mtumwa Ali Khamis ambae alishiriki katika mchezo wa kuigiza  wakati wa Shukrani na Pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar zilizotolewa na Wazee waliotimiza umri wa miaka 70 katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 12/07/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa wazee waliotimiza umri wa miaka 70 katika hafla maalum ya ilyofanyika kumpongeza yeye Rais iliyofanywa na Wazee hao katiika Viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 12/07/2016

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.