Habari za Punde

ZLSC Yatowa Elimu ya Uraia kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kisiwani Pemba.


Kaimu Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Ndg.Khalfan Amour Mohamed, akizungumza wakati wa mafunzo hayo ya elimu ya uraia kwa wanafunzi wa skuli za sekondari za mkoa wa kaskazini Pemba yaliofanyika afisini kwao mjini Chakechake.

Afisa wa Elimu skuli za sekondari mkoa wa kaskazini Pemba,Ndg. Said Massoud Othman akifungua mafunzo ya elimu ya uraia kwa wanafunzi wa skuli za sekondari za mkoa huo, yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba

Wanafunzi wa skuli za sekondari za mkoa wa kaskazini Pemba, wakiwa kwenye mafunzo ya elimu ya uraia yalioendeshwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, yaliofanyika afisini kwao mjini Chakechake
Mtoa Mada Ndg.Mohamed Hassan Ali Kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, akiwasilisha mada juu ya umuhimu na nafasi ya elimu ya uraia kwa wanafunzi, kwenye mafunzo yalioandaliwa na ZLSC na kufanyika afisini kwao mjini Chakechake

Mwanafunzi wa sekondari kutoka mkoa wa kaskazini Pemba, ambae hakupatikana jina lake akichangia jambo kwenye mafunzo ya elimu ya uraia yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.