MENEJA wa Hoteli ya Mbuyu Mkavu iliyoko Vitongoji
Wilaya ya Chake Chake, Abdalla Said ambaye ni muwekazaji mzalendo wa ndani,
akieleza matatizo yaliyopelekea kuifunga hoteli yake, katika kikao cha pamoja
na viongozi wa kamisheni ya Utalii Pemba, wa kwanza kulia ni mdhamini wa
kamisheni hiyo Suleiman Amour Suleiman.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA).
SEHEMU ya kupatia chakula wageni wanaofika katika
hoteli ya Mbuyu Mkavu iliyoko Vitongoji Wilaya ya Chake Chake Pemba, hoteli
hiyo kwa sasa imefungwa kutokana na changamoto za umeme kutokuwepo hotelini
hapo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).
IPO haja kwa watembeza watalii Kisiwani Pemba,
kuwafahamisha wageni wao jinsi wanavyotakiwa kutembea kwa kufuata mila na silka
za wananchi wa kisiwa cha Pemba, pichani watalii wakiwa katika mji wa chake
chake bila ya kujistiri katika miili yao.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA).
MDHAMINI wa Kamisheni ya Utali Kisiwani Pemba,
Mwalimu Suleiman Amour Suleiman wa kwanza kulia, akikagua buku la wageni katika
moja ya hoteli za kitalii zinazolaza wageni ndani ya Wilaya ya Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).
No comments:
Post a Comment