Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali vya Redio za FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 02/08/2016.
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Redio za FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 mwaka huu (kushoto) Naibu Katibu wa Rais Nd,Marium Haji Mrisho na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji,[Picha na Ikulu.] 02/08/2016.
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (kulia) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Redioza FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 mwaka huu (kushoto) Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji,[Picha na Ikulu.] 02/08/2016.
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 2.8.2016
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar zinatambua mchango mkubwa wa Wanadiaspora na ndio maana hutayarisha makongamano
ambayo hutoa fursa ya kujadili masuala mbali mbali ya kimaendeleo kwa lengo la
kuimarisha uchumi wa Tanzania na ustawi wa wananchi wake.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Salum
Maulid Salum aliyasema hayo leo huko Ikulu Mjini Zanzibar wakati alipofanya
mazungumzo na waandishi wa Habari mbali mbali kutoka Redio za FM zinazofanya
kazi zake hapa Zanzibar kuhusu Kongamano la Diapora la Tanzania linalotarajiwa
kufanyika hapa Zanzibar mwaka huu.
Katika maelezo yake Katibu Mkuu huyo
aliyekuwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Silima Kombo Haji, alisema kuwa kwa miaka miwili iliyopita
makongamano hayo yamefanyika Dar-es-Salam na kusisitiza kuwa mikutano
iliyokwisha fanyika imeweza kuleta mafanikio makubwa.
Alisema kuwa Mkutano wa mwaka huu unatarajiwa
kufanyika hapa Zanzibar kwa muda wa siku mbili kati ya tarehe 24 na 25
linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John
Pombe Magufuli huko katika ukumbi wa hoteli ya
Zanzibar Beach Resort.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa mada mbali
mbali zinatarajiwa kutolewa katika Kongamano hilo ambalo kauli mbiu yake ya kila mwaka ni “Mtu kwao
ndio Ngao’ ambapo pia, ujumbe mkubwa kwa mwaka huu ni “Mtizamo mpya wa
Kuimarisha Utalii wa Tanzania na uekezaji”.
Katika melezo yake Katibu Salum alisema
kuwa tayari matayarisho ya kongamano huo yanaendelea vizuri na kueleza kuwa
Wanadiaspora wamekuwa na mwamko mkubwa katika ushiriki ambapo kila mwaka idadi
ya ushiriki wao imekuwa ikiongezeka huku akieleza kuwa vyombo vya habari
zikiwemo Redio za FM, vina nafasi kubwa katika kuwaeleza wananchi juu ya mkutano
huo.
Aidha, alisema kuwa miongoni mwa
mafanikio yaliopatikana ni pamoja na Wanadiaspora wengi wa hapa nchini wameweza
kutoa michango yao mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha mirado mbali mbali
ya maendeleo ikiwemo ya afya, elimu na mengineyo.
Katibu Mkuu huyo alitumia fursa hiyo
kueleza juhudi za viongozi hapa nchin i katika kuhakikisha suala hilo
linaimarika huku akitolea mfano juhudi za makusudi zinazochukuliwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika
kuhakikisha ushirikiano kati ya Wanadiaspora na Serikali zote mbili unaimarika.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji aliwaeleza
waandishi hao wa habari faida zinazopatikana kutokana na kuunganishwa kwa
Wanadiaspora hapa nchini pamoja na changamoto zilizopo.
Balozi Silima alizitaja baadhi ya nchi
zilizopo ndani na nje ya Afrika ambazo zimenufaika na zinazaendelea kunufaika
kutokana na Wanadiaspora wa nchi zao zikiwemo Kenya, Ethiopia, Ghanam Idia,
Pakistan, Ufilipino, Bangladesh na nyenginezo.
Sambamba na hayo, Balozi Silima alisema
kuwa serikali zote mbili zimeweka mikakati maalum ya kuhakikisha Wanadiaspora
wanapewa kipaumbele sambamba na kushirikishwa katika masuala mbali mbali ya
maendeleo kwa nchi yao.
Rajab Mkasaba,
Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment