Habari za Punde

Kuwasili kwa Madawati Yaliotolewa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa Wabunge kwa Ajili ya Majimbo yao

Mwenyekiti wa Kamati ya Kutafuta Madawati Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman akiwa na Kamishna wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe Salim Turky(Mr White) wakiwa katika bandari ya Zanzibar kupokea madawati hayo yaliotolewa na Bunge kwa Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kila Mbunge amekabidhiwa madawadi 300 kwa Jimbo lake kwa ajili ya matumizi ya Skuli za Jimbo lake.
Kamishna wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe Salim Turky(Mr.White) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi madawati hayo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kuchangia Madawati Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman. na kusema madawati haya yamenunuliwa na fedha zilizobakia katika bajeti iliopita kwa Zanzibar wamepata mgao wa madawti 5500, kilaq Mbunge amepata Madawati 300, kwa Majimbo ya Ungja na Pemba. 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kuchangia Madawati Zanzibar Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akitowa shukrani kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msaada huu wa Madawati kwa Skuli za Zanzibar kupitia kwa Wabunge wa Majimbo husika.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Znzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akitowa shukrani kwa Serikali ya Muungano wa Tanzania kwa msaada huu wa madawati na kuwataka Taasisi nyengine kuiga mfano huu wa kuchangia madawti kwa ajili ya Watoto wetu kuweza kupata Elimu Bora. Kamishna wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe Salim Turky (Mr White) akimkabidhi madawati Mwenyekiti wa Kamati ya Kuchangia Madawati Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman kwa ajili ya Skuli za Majimbo ya Zanzibar yaliotolewa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo imefanyika katika bandari ya malindi Zanzibar baada ya kuwasili kutokea Tanzania Bara na Meli ya Kampuni ya Azam Marine. 
 Baadhi ya Madawati 550 ya Majimbo ya Unguja na Pemba yakiwa katika Bandari ya Malindi Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Welezo Zanzibar Mhe Saada Mkuya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi madawati kwa Wabunge wa Zanzibar katika bandari ya malindi Zanzibar.  
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuchangia Madawati Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Riziki Pembe Juma wakati wa hafla hiyo 
 Kamati ya Kuchangia Madawti Zanzibar wakizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe Salim Turky.
Baadhi ya Madawati 550 yakiwa katika bandari ya malinzi Zanzibar baada ya kuwasili na kugawiwa kwa Waheshimiwa wabunge kwa ajili ya Skuli za Majimbo yao. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.