Habari za Punde

Simba Wawatilisha Saini Watano

KLABU ya Simba imekamilisha usajili wa wachezaji wa kimataifa kwa kuwasainisha mikataba tayari kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baadaye mwezi huu. 

Simba inatarajia kukitambulisha rasmi kikosi chake kwenye sherehe maalum zizofanyika Agosti 8 kila mwaka maarufu kama Simba Day zitakazofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 

Wachezaji hao wanaungana na mlinda mlango Vicent Agban kutoka Ivory Coast pamoja na mlinzi wa kati Juuko Murshid wa Uganda kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni. 
Sherehe za Simba Day msimu huu zinakwenda sambamba na sherehe za miaka 80 tangu kuanzishwa kwake. 

Wachezaji waliosaini mikataba kuichezea Simba ni Method Mwanjale, Musa Ndusha, Janvier Bokungu, Fredric Blagnon na Laudit Mavugo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.