Habari za Punde

Timu yac Azam Yawachomoa Mabeki Kisiki.

Klabu ya Azam imeingia mkataba na walinzi wawili, Daniel Amoah wa Ghana na Bruce Kangwa kutoka Zimbabwe, kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao. 


Wawili hao kila mmoja amesaini mkataba wa miaka mitatu. 
Amoah anayecheza nafasi ya mlinzi wa kati amesajiliwa akitokea klabu ya Medeama ya Ghana, wakati Kangwa aliyefuzu majaribio ya kujiunga na Azam FC akitokea kwa vinara wa Ligi Kuu Zimbabwe, Highlanders. 

Klabu ya Ndanda ya mjini Mtwara imefanikiwa kuwasajili kwa mkopo Braison Raphael na Abdallah Heri kutoka Azam FC kwa ajili kujiimarisha zaidi kueleka msimu mpya wa VPL.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.